Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
11 Mei 2020 19:11:48
Spironolactone (Aldactone)
Spironolactone ni dawa mojawapo inayotumika kushusha shinikizo la juu la damu iliyo kundi la Potasiamu sparing diuretic.
Majina ya kibiashara
Spironolactone hufahamika kwa jina jingine la Aldactone.
Fomu na dozi ya Spironolactone
Spironolactone hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa;
25 mg
50 mg
100 mg
Ufanyaji kazi wa Spironolactone
Dawa jamii ya Potasiamu Sparing Diuretic ikiwa pamoja na Spironolactone hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu ;
Hufanya kazi kwa kuzuia utendaji kazi wa homoni ya Aldosterone ambayo hufanya kazi ya kuthibiti kiasi cha sodiamu na maji kwenye damu. Kuzuia utendaji kazi wa homoni hii husababisha kupotea sana kwa maji na chumvi mwilini kwa njia ya mkojo hivyo kupunguza kiwango cha damu katika mishipa ya damu na shinikizo la damu ndani ya mishipa. Dawa hii pia huzuia kupotea kwa kiwango cha potasiamu kwenye damu, hii ndo maana jina la kundi hili limeitwa potasiamu sparing diuretics
Dawa kundi moja na Spironolactone
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na dawa hii ni;
Triamterene
Amiloride
Eplerenone
Spironolactone hutibu nini
Hutumika kwa matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la juu la damu
Hutumika kwa matibabu ya wagonjwa wa anjaina
Hutumika kwa matibabu ya wagonjwa wa moyo ulioferi dalaja la iii na iv
Hutumika kwa matibabu ya wagonjwa wa ini lililosinjaa (sirosisi)
Hutumika kwa matibabu ya wagonjwa wenye kiwango cha chini cha potasiamu (Haipokalemia)
Upekee wa Spironolactone
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili ni;
Dawa hii huchukua muda mrefu zaidi ili kutenda kazi ukilinganisha na dawa zingine kwenye kundi hili
Mwingiliano wa Spironolactone na dawa zingine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Amiloride
Drospironone
Eplerenone
Triamterene
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Spironolactone
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au zingine katika kundi lake
Wagonjwa wenye ugonjwa wa Addison
Angalizo
Tahadhari ya Spironolactone
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo
Nusu maisha na umetaboliwa Spironolactone
Dawa hii baada ya kutumiwa hufikia kileleni kwenye damu damu ndani ya saa moja na kudumu mwilini kwa saa 1.3 hadi 11.2. Mabaki ya dawa hutolewa kwa njia ya Mkojo kwa asilimia 47 hadi 57 na kinyesi kwa asilimia 35 hadi 41.
Matumizi ya Spironolactone wa mama mjamzito
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito endapo faida ni nyingi kuzidi hatari
Matumizi ya Spironolactone kwa mama anayenyonyesha
Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha sababu huenekana kwenye maziwa baada ya kutumia dawa hii
Maudhi ya Spironolactone
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ini;
Kutapika
Haipokalemia
Matiti kuuma
Kizunguzungu
Kichefuchefu
Kuwashwa mwili
Maumivu ya tumbo
Maumivu ya kichwa
Kupata vipele kwenye Ngozi
Mwili kukosa nguvu
Mambo mengine ya kufahamu mgonjwa
Mgonjwa anatakiwa kushauriwa kutotumia dawa zingine za kuongeza madini ya potasiamu au vyakula vyenye potasiamu kwa wingi ikiwa pamoja na chumvi.
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako ya Spironolacton, tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana, subiria muda huo ufike kasha kunywa dozi hiyo moja na endelea kama ulivyoshauriwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:55
Rejea za mada hii:-