top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

27 Mei 2020 05:35:05

Troglitazone

Troglitazone

Troglitazone ni dawa mojawapo iliyokuwa ikitumika kutibu ugonjwa wa kisukari aina ya pili iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa thiazolidinedione.


Majina ya kibiashara


Troglitazone huwa maarufu kwa jina Rezulin


Fomu ya dawa


Troglitazone hupatikana katika mfumo wa kidonge.


Troglitazone bado inatumika?


Kwa sasa dawa hii imeondolewa kwenye soko la dawa duniani sababu huweza kuathiri ini na kupelekea kifo.


Namna Troglitazone inavyofanya kazi


Dawa jamii ya thiazolidinedione ikiwa pamoja na Trosiglitazone hufanya kazi zifuatazo ili kuthibiti kiasi cha sukari mwilini;


Huchochea risepta za Peroxisome Proliferator ili zizalishe homoni insulin kwa wingi inayofanya kazi ya kuongeza matumizi ya sukari kwenye seli na kubadikubadilisha kiasi cha sukari iliyozidi kwenye damu kuwa glaikogen.


Dawa zilizo kundi sawa na Troglitazone


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Kundi la thiazolidinedione) na dawa hii ni;


 • Rosiglitazone

 • Pioglitazone


Troglitazone ilikuwa ikitumika kutibu nini?


Troglitazone ilikuwa ikitumika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu kwa wagonjwa wenye Kisukari aina ya pili


Upekee wa Troglitazone


Utofauti wa pekee wa Troglitazone na dawa zingine za kwenye kundi hili la thiazolidinedione

Dawa hii huweza kuwa sumu kwenye ini na kupelekea kifo


Troglitazone ilikuwa haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;

 • Baricitinib

 • Eluxadoline

 • Gemfibrozil

 • Ethanol


Wagonjwa waliokuwa hawapaswi kutumia Troglitazone


Troglitazone ilikuwa haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;


 • Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au dawa zingine jamii ya thiazolidinedione

 • Wagonjwa wenye moyo ulioferi


Angalizo


Tahadhari ya Troglitazone


 • Huweza kupelekea kuongezeka kwa uzito inapotumika pamoja na dawa zingine za kumeza za kutibu kisukari

 • Ni sumu kwa ini na huweza kusababisha kifo

 • Huweza kupelekea kuvimba


Matumizi ya Troglitazone kwa mama mjamzito


Tafiti kwenye zilizofanyika kwa wanyama zinaonyesha kuwepo kwa madhara katika ukuaji wa mtoto ilipotolewa kwenye panya na sungura wenye mimba, hivyo haipaswi kutumika kwa kwa mama mjamzito.


Matumizi ya Troglitazone kwa mama anayenyonyesha


Haipaswi kutumika kwa mama anayenyonyesha kutokana na athari zake kwenye ini.

Huweza kupelekea ini la mtoto kupata sumu na kupelekea kifo


Maudhi ya Troglitazone


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;


 • Shinikizo la juu la damu

 • Moyo kuferi

 • Kuharisha

 • Maambukizi ya juu ya mfumo wa upumuaji

 • Kichwa kuuma

 • Sukari kushuka

 • Maumivu ya misuli


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako kunywa mara pale utakapo kumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:55

Rejea za mada hii:-

1.Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasawa 776

2.DrugBank.Troglitazone.https://www.drugbank.ca/drugs/DB00197.Imechukuliwa 4/5/2020

3.ScienceDirect.Troglitazone.https://www.sciencedirect.com/topics/neuroscience/troglitazone .Imechukuliwa 4/5/2020

4.Drugs.Troglitazone.https://www.drugs.com/mtm/troglitazone.html.Imechukuliwa 4/5/2020

5.Ncbi.Troglitazone.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK548142/.Imechukuliwa 4/5/2020
bottom of page