Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
31 Mei 2020 15:18:44
Valsartan
Valsartan ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu katika kundi la dawa linaloitwa angiotensini II risepta antagonist (ARBs).
Majina ya kibiashara
Valsartan huwa maarufu pia kwa jina la
Diovan au
Prexxartan.
Fomu na uzito wa Valsartan
Valsartan hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa ;
40mg
80mg
160mg na
320mg
Valsartan hupatikana katika mfumo wa maji wenye ujazo wa miligramu 4 kwa mililita (4mg/ml)
Ufanyaji kazi wa Valsartan
Dawa jamii ya ARBs ikiwa pamoja na Valsartan hufanya kazi zifuatvyo ili kupunguza shinikizo la damu.
Hufanya kazi kwa kufunga risepta za Angiotensin II zijulikanazo kama AT1 Risepta, risepta za AT1 hupatikana kwenye moyo,mishipa ya damu na figo. Vipokezi hivi vinapofungwa hupelekea Kutanuka kwa mishipa ya damu na kuwa na kipenyo kikubwa na kupelekea kushuka kwa shinikizo la damu
Hupinga uzalishwaji wa homoni ya Aldosterone ambayo hutumika kuthibiti kiasi cha sodiamu na maji, Kiasi cha sodiamu kinapothibitiwa husababisha kupungua kwa shinikizo la damu kwa kuwa chumvi na maji mwilini hupungua.
Dawa kundi moja na Valsartan
Valsartan ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:
Losartan ( Cozaar)
Azilisartan (Edarbi)
Candesartan (Atacand)
Eprosartan (Teveten)
Olmesartan (Benicar)
Telmisartan(Micardis)
Irbesartan (Avapro)
Valsartan hutibu nini?
Valsartan hutumika kushusha shinikizo la damu la juu
Mwingilino wa Valsartan na dawa zingine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Aliskiren
Apalutamide
Benazepril
Captopril
Enalapril
Erdafitinib
Fedratinib
Fosinopril
Idelalisib
Ivosidenib
Lisinopril
Lithium
Lofexidine
Moexipril
Perindopril
Quinapril
Ramipril
Siponimod
Trandolapril
Voxelotor
Nani hapaswi kutumia Valsartan?
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wenye mzio na dawa hii au dawa jamii ya ARBs
Angalizo
Valsartan inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye moyo kuferi (CHF)
Wagonjwa wenye riski ya kupata haipotesheni na haipokalemia
Wagonjwa wenye shida ya figo kuferi
Wagonjwa wenye shida ya anjioidima
Matumizi ya Valsartan kwa mama mjamzito
Haipaswi kutumika kwa mama mjamzito kwa sababu husababisha athari kwa mtoto.
Matumizi ya Valsartan kwa anayenyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa Valsartan kuingia au kuwa kwenye maziwa ya mtoto ila aishauriwi itumike kwa wamama wajawazito.
Upekee wa Valsartan
Valsartan baada ya kutumiwa huanza kazi yake baada ya masaa mawili na kufikia kilele kati ya masaa manne mpaka sita
Maudhi ya Valsartan
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Kizunguzungu
Maumivu ya kichwa
Haipotesheni
Maumivu ya tumbo upande wa juu
Kikohozi kikavu
Mwili kuchoka
Je kama umesahau dozi yako ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi yako ya Valsartan, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:55
Rejea za mada hii:-