Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
18 Aprili 2020 19:18:37
Vildaglipitin
Ni dawa ya inayotumika katika tiba ya ugonjwa wa kisukari aina ya pili, ipo kwenye kundi la dawa linaloitwa dipeptidyl peptidase-4 (DPP-4).
Majina ya kibiashara
Vildaglipitin hufahamika kwa majina mengine ya kibiashara kama Galvus.
Dawa zilizo kundi moja na Vildaglipitin
Saxagliptin
sitagliptin
Alogliptin
Linagliptin
Jinsi Vildaglipitin inavyofanya kazi
Hufanya kazi kwa kuongeza kiasi cha homoni za kimetaboli zinazoitwa inkretin ambazo huthibiti kiwango cha glukosi kwenye damu kwa kuchochea kuzalishwa zaidi kwa homoni ya Insulin, hasa baada ya kula
Hupunguza kiasi cha sukari kinazalishwa na ini kisha kuingia kwenye damu.
Vildaglipitin hutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya kisukari aina ya pili
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Vildaglipitin
Metformin
Pioglitazone
Glyburide
Simvastatin
Amlodipine
Valsartan
Ramipril
Digoxin
Warfarin
Angalizo
Tahadhari ya Vildaglipitin kwa wagonjwa wenye mzio na dawa hii.
Matumizi ya Vildaglipitin Kwa mama mjamzito
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito
Matumizi ya Vildaglipitin kwa mama anayenyonyesha
Hakuna athari zozote zinazoweza kutokea kwa mtoto zinapotumiwa na mama anayenyonyesha.
Maudhi ya Vildaglipitin
Maudhi madogo ya Vildaglipitin ni;
Maumivu ya kichwa
Nasofarinjaitizi
Konstipesheni(haja kubwa ngumu)
Kizunguzungu
Kutokwa na jasho sana
Je endapo umesahau dozi ya Vildaglipitin ufanyeje?
Kama umesahau dozi yako ya Vildaglipitin, tumia mara pale utakapokumbuka isipokuwa muda wa dozi nyingine umekaribia sana, ruka dozi hiyo kasha endelea na dozi imayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:21:57
Rejea za mada hii:-