top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Sospeter M, MD

Dkt. Lugonda B, MD

2 Aprili 2026, 11:54:28

Zaha 500mg

Zaha 500mg

Zaha ni nini?

Zaha 500mg ni jina la kibiashara ambalo asili yake ni dawa Azithromycin.


Zaha 500 mg humaanisha nini?

Zaha 500mg humaanisha kidonge cha Azithromycin chenye uzito wa miligram 500.


Zaha inatibu nini?

Zaha ni antibiotic inayotumika kutibu aina mbalimbali za maambukizi ya bakteria wanaodhuriwa na dawa hii kwenye mfumo wa upumuaji, sikio, pua, koo, mapafu, ngozi na macho kwa watu wazima na watoto. Pia inafaa katika homa ya matumbo na baadhi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono.


Zaha inatumika yenyewe kutibu magonjwa?

Zaha/Azithromycin inaweza kutumika yenyewe au pamoja na dawa zingine kutibu magonjwa yaliyoorodheshwa hapo juu. Unapaswa kuwasiliana na daktari kwa vipimo na ushauri zaidi ili kufahamu kama dawa inauwezo wa kutibu maradhi yako.


Wapi unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu zaha?

Kusoma zaidi kuhusu zaha kwenye mada ya Azithromycin.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 11:54:28

Rejea za mada hii:-

<ol class="font_8">
<li><p class="font_8">ZAHA 500mg. https://www.1mg.com/drugs/zaha-500mg-tablet-701077. Imechukuliwa 10.06.2021</p></li>
<li><p class="font_8">ZAHA 500mg. https://www.1mg.com/drugs/zaha-500mg-tablet-701077. Imechukuliwa 10.06.2021</p></li>
</ol>
bottom of page