top of page

Dawa za kutibu haja ngumu- konstipesheni

 

Konstipesheni ni kupata haja kubwa isiyoridhisha, hii huweza kuwa kwa sababu ya kutokwenda choo kwa idadi inayotakiwa, kushindwa kutoa choo kiurahisi au kuhisi umeshindwa kutoa choo chote. Tatizo hili huwez akutokea kwenye umri wowote ule lakini hutokea sana kwa wanawake watu wazima, wazee na wakati wa ujauzito. Ni muhimu kwa wanaolalamika kupata konstipesheni kuzingatia kuhusu hali zao halisi kwa sababu kila mtu hutofautiana tabia ya kwenda choo na mtu mwingine, baadhi ya watu hupata choo kila siku. Endapo dalili zinazoambatana ni upungufu wa damu, damu kwenye kinyesi, maumivu ya tumbo, kupungua uzito na una miaka zaidi ya 50, utahitajiuchunguzi wa haraka ili kujua shida ni nini

​

Matibabu

 

Kwa wagonjwa wote wenye tatizo la haja ngumu, matibabu ya kuongeza kiwango cha maji unayokunywa na vyakula vyenye nyuzinyuzi bado hubaki jambo la kwanza kabisa katika sehemu ya matibabu. Utumiaji wa vyakula vyenye nyuzinyuzi unatakiwa kuwa wa kuongezeka taratibu na si ghafla ili kupinguza kupata gesi tumboni na hisia za kushiba. Matunda yenye kiwango cha nyuzinyuzi kwa wingi na juisi zenye sorbitol huwez akufanya kazi nzuri ya kuondoa tatizo la konstipesheni. Hata hivyo matumizi ya vyakula vyenye nyuzi kwa wingi huweza kufnaya kazi baada ya wiki zisizozidi 4.

​

Matumizi ya dawa za kufanya uharishe huweza kupelekea upoteze madini muhimu mwilini, matumizi haya hutokana na elimu duni ya anayetoa dawa hizi kwa kutoelewa ni nini haswa kinachosababisha konstipesheni. Sababu ya msingi inayopelekea konstipesheni inatakiwa tambuliwa na kutibiwa  kabla ya  kumpa dawa mgonjwa.

​

Dawa

  • Ispaghula husk

  • Methylcellulose

  • Sterculia

  • Docusate sodium

  • Co-danthramer na Co-danthrusate

 

Dawa za kulainisha haja ngumu

 

  • Docusate sodium

  • Glycerol supozitorizi

  • Enema ya mafuta ya karanga na peanut

​

Dawa za kuongeza maji kwenye kinyesi

  • Lactulose

  • Macrogols

  • Guanylate cyclase-C risepta agonist

  • Lubiprostone

  • Prucalopride

 

Konstipesheni ilosababishwa na

  • Docusate sodium

  • Naloxegol

  • Methylnaltrexone bromide

 

Haja kuziba

  • Enema ya Sodium citrate

  • Glycerol

  • Macrogol

  • Sodium acid phosphate

 

Konstipesheni sugu

  • Macrogols

  • Prucalopride

  • Lubiprostone

  • Bisacodyl

  • Potassium chloride

  • Sodium bicarbonate

  • Sodium chloride

 

Feko impaction kwa watoto

  • Ispaghula husk

  • Methylcellulose

  • Sterculia

  • Lubiprostone

  • Lactulose

  • Macrogol 3350

  • Sterculia

bottom of page