top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

2 Aprili 2026, 11:44:17

Image-empty-state.png

Acamprosate na ujauzito

Imeboreshwa:

Kwenye tafiti zilizoanyikwa kwa panya, inayonyesha kuwa acamprosate ilikuwa sumu kweney uumbaji wa kijusi kwenye dozi ya kawaida anayoweza kutumia binadamu. Matatizo yaliyokuwa yanatokea kwa panya ni pamoja na kutofanyika vema kwa Iris, kuzaliwa na madhaifu ya macho na madhaifu kuhama sehemu yake asili mshipa wa damu wa subclavian artery. Hakuna tafiti zilizofanyika kwa binadamu kwa kuwa dawa hii ni sumu kwa binadamu.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha Hatari kubwa


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha Hatari kubwa , ina maana gani?

Inawezekana kuwa hakuna taarifa za uzoefu kwa matumizi kwa binadamu au taarifa chache zilizopo zinaonyesha kutohusiana na matatizo ya kiuumbaji kwa mtoto kama madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika. Dawa hii inasababisha sumu kwa kwenye ukuaji wa kijusi cha wanyama wa jamii mbili au tatu waliopewa dawa hii kwenye dozi ambayo haisababishi sumu kwa mama mjamzito, dozi iliyo chini ya mara kumu ya dozi ya binadamu, dozi inayotolewa kuendana na jumla ya eneo la mwili


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji,ina maana gani?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 11:41:58

Rejea za dawa

1. Product information. Campral. Forest Pharmaceuticals, 2012.

bottom of page