Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
2 Aprili 2026, 11:45:46
Bacitracin na ujauzito
Imeboreshwa:
Taarifa za dawa ya bacitracin wakati wa ujauzito ni chache, hata hivyo inawezekana hakuna hatari ya madhara kiuumbaji kwa kichanga kwa anayetumia dawa ya kupaka. Dawa ya kuchoma haijaruhusiwa kutumika kwa watu wazima na haitakiwi kutumikakwa wajawazito
Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito
Inapatana na ujauzito (Dawa ya kupaka)
Inapatana na ujauzito maana yake nini?
Uzoefu wa matumizi kwa binadamu kuhusu dawa hii au dawa zingine zilizo kundi moja au zenye kufanya kazi kwa utaratibu unaofanana, zinatosha kuonyesha kuwa, madhara kwa kichanga tumboni ni madogo sana au hakuna kabisa. Tafiti za uzazi kwa wanyama hazina uhalisia kwa binadamu.
Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha
Inapatana na kunyonyesha (dawa ya kupaka tu)
Inapatana na kunyonyesha maana yake nini?
Kiasi kidogo cha dawa hii kinawezekana kuingia kwenye maziwa ya mama, kiasi hiki hakina mashiko ya kusababisha sumu kwa kichanga anayenyonya. Dawa hii haitarajiwi kusababisha madhara kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa hii.
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 11:41:58
Rejea za dawa
Heinonen OP, Slone D, Shapiro S. Birth Defects and Drugs in Pregnancy. Littleton, MA: Publishing Sciences Group; 1977. p. 297, 301.
