top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin S, MD, Dkt. Adolf S, MD.

18 Aprili 2025, 15:23:36

Image-empty-state.png

Dalili za mimba ya miezi kumi

Imeboreshwa:

Utangulizi

Mimba ya miezi kumi ni sawa na mimba ya wiki 37 hadi 40. Ingawa watu wengi hufahamu kuwa binadamu hubeba ujauzito kwa miezi tisa, ukweli ni kwamba hudumu kwa miezi 10. Hii ni kwasababu umri wa ujauzito huhesabiwa kuanzia tarehe ya kipindi cha mwisho cha hedhi (LMP). Hii huongeza takriban wiki 2 kwenye muda wa jumla wa ujauzito, kwa kuwa ovulesheni na utungwaji mimba hutokea wiki mbili baada ya LMP na kufanya kufikia wiki 40 ambazo ni miezi 10.


Hiki ni kipidni cha mwisho kabisa cha ujauzito na mtoto huwa katika ukamilifu wa kuzaliwa. Ni muhimu kuelewa dalili, hatari zinazoweza kutokea, na matunzo ya kiafya yanayohitajika katika kipindi hiki ili kuhakikisha usalama wa mama na mtoto.


Je, ni zipi dalili za mimba ya miezi kumi?

Miongoni mwa dalili za kawaida zinazoweza kuonekana ni pamoja na;

  • Kuhisi mtoto akicheza kwa nguvu zaidi: Unaweza kuhisi mtoto akirusha miguu na mikono kwa nguvu au mara kwa mara

  • Mikazo ya uchungu wa uongo: Hii ni mikazo ya majaribio ambayo huashiria kuwa mwili unajiandaa kwa uchungu wa kujifungua

  • Mgandamizo mkubwa katika nyonga: Mtoto anaposhuka kuelekea nyongani, mama anaweza kuhisi msukumo au maumivu.

  • Kukosa usingizi: Mabadiliko ya kihisia, kukojoa mara kwa mara na mawazo ya kujifungua, usingizi unaweza kuathirika

  • Maumivu ya mgongo na viungo: Maumivu haya huongezeka kutokana na uzito wa mtoto na mabadiliko ya homoni.


Mambo ya kuzingatia

Kipindi cha ujauzito kilichopita muda wake kinahitaji uangalizi wa karibu. Mambo muhimu ya kuzingatia ni:

  • Hakikisha umekamilisha mpango wa kujifungua na umshirikishe mtoa huduma wako wa afya     

  • Hakikisha vifaa vya kujifungulia vipo tayari

  • Anza au endelea kufanya mazoezi mepesi ya kuandaa nyonga kwa ajili ya leba


Je, ni wakati gani unapaswa kumuona daktari?

Unapaswa kumwona daktari haraka endapo:

  • Unahisi mtoto hachezi kama kawaida

  • Unahisi maumivu makali tumboni

  • Kutoka damu au maji ukeni

  • Dalili za uchungu wa uzazi  kama vile mikazo ya mara kwa mara, kuvunjika kwa chupa ya uzazi, au maumivu ya mgongo yanayoendelea.

  • Hakuna dalili za kujifungua hadi wiki 41–42

  • Dalili za ghafla au kali Kama maumivu ya kichwa, mabadiliko ya kuona, au uvimbe, ambavyo vinaweza kuashiria kifafa cha mimba


Wapi utapata maelezo zaidi kuhusu mimba ya miezi kumi?

Ili  kupata maelezo zaidi kuhusu mimba ya miezi kumi bofya hapa.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeandikwa:

18 Aprili 2025, 11:40:49

Rejea za dawa

  1. American College of Obstetricians and Gynecologists. (2020). Practice bulletin no. 222: Gestational hypertension and preeclampsia. Obstetrics & Gynecology, 135(6), e237–e260.

  2. Brancazio, L., & Wang, C. (2018). Sleep disorders in pregnancy. Obstetrics and Gynecology Clinics of North America, 45(3), 533–548.

  3. Cunningham, F. G., Leveno, K. J., Bloom, S. L., Spong, C. Y., Dashe, J. S., Hoffman, B. L., Casey, B. M., & Sheffield, J. S. (2018). Williams obstetrics (25th ed.). McGraw‑Hill Education.

  4. Rich‑Edwards, J. W., Kleinman, K., Abrams, A., Harlow, B. L., McLaughlin, T. J., Joffe, H., & Gillman, M. W. (2006). Sociodemographic predictors of antenatal and postpartum depressive symptoms. Journal of Epidemiology & Community Health, 60(3), 221–227. https://doi.org/10.1136/jech.2005.038758

  5. Ueland, K., Hanevik, H. S., Sommerseth, H., & Andersson, E. (2015). Sleep patterns and problems in the third trimester of pregnancy: A cohort study. Sleep Medicine Reviews, 19, 47–59.

bottom of page