top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin S, MD, Dkt. Adolf S, MD.

18 Aprili 2025, 15:18:42

Image-empty-state.png

Dalili za Mimba ya Miezi Mitatu

Imeboreshwa:

Utangulizi

Mimba ya miezi mitatu ni sawa na mimba ya wiki 9 hadi 12. Kufikia mwezi wa tatu wa ujauzito inaashiria mwisho wa kipindi cha kwanza cha ujauzito.


Kipindi hiki kinaweza kuleta mchanganyiko wa dalili zilizokuwepo awali na zingine mpya. Kujua dalili unazoweza kutarajia kunaweza kukusaidia kujihisi salama na tayari kwa hatua zinazofuata.

 

Je, ni zipi dalili za mimba ya miezi mitatu?

Zifuatazo ni  dalili ambazo wanawake wengi hupitia wakati huu:

  • Kichefuchefu na kutapika: Kichefuchefu na kutapika bado vinaweza kuendelea, lakini vinaweza kupungua kadri mwezi huu unavyosonga.

  • Mwili kuchoka: kuhisi kuchoka sana bado ni kawaida, kwani mwili wako unatumia nguvu nyingi.

  • Kukojoa mara kwa mara: kutanuka kwa kizazi huleta mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo, hivyo kwenda chooni mara kwa mara ni jambo la kawaida.

  • Mabadiliko ya matiti: Matiti yanaweza kuwa laini, kuvimba au kuona rangi eneo jeusi kuzunguka chuchu likiongezeka kuwa jeusi tofauti na awali

  • Mabadiliko ya hisia: Homoni zinazobadilika zinaweza kusababisha kuhisi furaha, huzuni au hasira ghafla.

  • Hali ya kubagua vyakula: Inawezekana ukapenda chakula fulani sana au kuchukia harufu au ladha ya vingine.

  • Mishipa ya damu kuonekana zaidi: Kuongezeka kwa damu mwilini kunaweza kufanya mishipa ya damu kuonekana wazi chini ya ngozi.

 

Mambo ya kuzingatia

  • Pata muda wa kupumzika, kula chakula bora na kunywa maji ya kutosha.

  • Hudhuria kliniki ya ujauzito kwa kufuata miadi unayopewa

  • Ukihisi dalili kali au zisizo za kawaida, wasiliana na mtoa huduma wa afya mara moja.


Je, ni wakati gani unapaswa kumuona daktari?

unapaswa kumuona daktari endapo utaona miongoni mwa dalili hizi:

  • Maumivu makali ya tumbo

  • Kutokwa na damu ukeni

  • Kichefuchefu na kutapika kupita kiasi

  • Maumivu au kuwashwa wakati wa kukojoa

  • Kizunguzungu kikali au kupoteza fahamu

  • Uvimbaji wa ghafla wa mikono, miguu, au uso

  • Maumivu makali ya kichwa au mabadiliko ya kuona


Wapi utapata maelezo zaidi kuhusu mimba ya miezi mitatu?

Ili  kupata maelezo zaidi kuhusu mimba ya miezi mitatu bofya hapa.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeandikwa:

10 Aprili 2025, 09:28:14

Rejea za dawa

  1. MSD Manuals. (2024). Physical changes during pregnancy - Women's health issues. https://www.msdmanuals.com/home/women-s-health-issues/normal-pregnancy/physical-changes-during-pregnancy . Imechukuliwa 10.04.2025

  2. Healthline. (2020). 3 months pregnant: Symptoms, belly, baby's development, more. https://www.healthline.com/health/pregnancy/3-months-pregnant#takeaway. Imechukuliwa 10.04.2025

  3. National Health Service. (2023). You and your baby at 12 weeks pregnant. https://www.nhs.uk/pregnancy/week-by-week/1-to-12/12-weeks/.  Imechukuliwa 10.04.2025

bottom of page