top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

2 Aprili 2026, 11:43:34

Image-empty-state.png

Levocetirizine na ujauzito

Imeboreshwa:

Hakuna ripoti zinazoelezea matumizi ya levocetirizine kwa binadamu mjamzito. Taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo kwa hatari kiasi, na hivyo kufanya kutowezekana kufahamu kuhusu madhara kwa ya kiuumbaji kwa kichanga. Hakuna taarifa zinazosema kwamba dawa jamii ya antihistamine pamoja na hii ni sumu ambayo inaweza pelekea kutokea kwa madhara ya kiuumbaji kwa kichanga tumboni. Licha ya hayo, endapo matumizi ya antihistamine yatahitajika wakati wa ujauzito, uchaguzi ni kutumia dawa zenye taarifa na zinappnekana kuwa afadhali zaidi kama vile chlorpheniramine au diphenhydramine.


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari kidogo


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari kidogo ina maana gani?

Inawezekana kuwa hakuna taarifa za zoefu wa matumizi ya dawa hii au taarifa za binadamu wajawazito wachache waliotumia dawa hii zimeonyesha kutohusiana kuwa sumu kwa kichangawa tumboni kuweza kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika. Dawa haileti sumu kwenye uumbaji wa kijusi( kwenye dozi ambayo haikusababisha sumu kwa mama) kwenye jamii zote za wanyama waliofanyiwa tafiti kwenye dozi ambayo ni sawa au pungufu ya mara kumi ya ile ya binadamu, dozi inayotolewa kuendana na jumla ya eneo la mwili


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inawezekana patana na unyonyeshaji ina maana gani?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 11:41:58

Rejea za dawa

  1. Product information. Xyzal. UCB; 2008.

  2. Product information. Xyzal. Sanofi-Aventis; 2008.

bottom of page