top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

6 Aprili 2026, 02:53:16

Image-empty-state.png

Upumuaji mzuri wakati wa ujauzito

Imeboreshwa:

Ukiwa kwenye hali ya kawaida, mjongeo wa kifua na upumuaji hufanyika kawaida kulinga na mahitaji ya mwili wako na unavyopenda. Wakati wa ujauzito, mtoto tumboni hukua na huchukua nafasi ya kutosha kiasi cha kupunguza nafasi kwa ajili ya kupumua vema. Hii ndo maana unaweza kuhisi kuishiwa pumzi wakati huu wa ujauzito.


Namna ya kutambua aina ya upumuaji wako kwenye ujauzito?


Endapo unataka kujua namna unavyopumua fanya yafuatayo;


  • Kaa pozi zuri lenye uhuru(Unaweza kukaa au kulala)

  • Weka mikono yako miwili eneo la chini ya mbavu/kifua

  • Vuta pumzi kupitia pua kiasi cha kusukuma mikono yako uliyoweka chini ya kifua kwa jinsi unavyoweza. Toa pumzi kupitia mdomo. Rudia zoezi hili mara tatu kwa siku.

  • Rudia zoezi hilo hapo juu wakati umeweka mikono kwenye tumbo


Madhara ya kuvuta pumzi vibaya wakati wa kujifungua


Ulipokuwa unavuta pumzi kwenye zoezi la hapo juu, kifua kilikuwa kinapanuka taratibu. Mijongeo ya kifua na tumbo ni muhimu sana wakati wa upumuaji wa kawaida. Kuvuta pumzi kunaweza kuwa hatari kwa mama na mtoto tumboni.


Hatari inatokea endapo

  • Unapopumua haraka haraka haswa wakati uchungu upo kileleni

  • Unaposimamisha pumzi

  • Kupumua haraka haraka na si kwa kina. Hii husababisha hewa kidogo kuingia kwenye mapafu na hupelekea haipoventilesheni

  • Kupumua taratibu na kwa kina huweza kusababisha haipaventilesheni na kupelekea kuhisi ganzi ya vitu kuchomachoma vidoleni.


Upumuaji wakati wa ujauzito na kujifungua


Wakati wa ujauzito na kujifungua, unahitajika kutilia umaanani kupumua kawaida. Wakati wa leba(uchungu) kila uchungu unavyotokea unatakiwa kuongeza upumuaji na kuvuta hewa kwa kina na kwa urahisi iwezekanavyo. Pumua kawaida bila kutumia nguvu za ziada.


Namna ya kupumua vema wakati wa kujifungua


Tumia pozi kama linaloonekana kwenye picha kisha pumua taratibu wakati unataka kuanza kufanya mazoezi yoyote yale.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeandikwa:

5 Aprili 2026, 06:34:16

Rejea za dawa

  1. American Pregnancy Association. Sleeping positions during pregnancy. Imechukuliwa 28.04.2020

  2. National Sleep Foundation. The best position for sleep during pregnancy.Imechukuliwa 28.04.2020

  3. National Posture Institute. Incorporating NPI’s 4 points of posture during pregnancy and postpartum. Imechukuliwa 28.04.2020

  4. https://www.pregnancyexercise.co.nz/products/fit2birthmum/. Imechukuliwa mara ya mwisho 3.06.2020

  5. Malposition and malpresentantio. https://www.gfmer.ch/Obstetrics_simplified/malpresentations_and_malposition.htm. Imechukuliwa 04.06.2020

  6. Ocipitalposterior.https://www.uptodate.com/contents/occiput-posterior-position. Imechukuliwa 04.06.2020

  7. Pushing the baby out.https://www.whattoexpect.com/pregnancy/labor-and-delivery/childbirth-stages/pushing-and-delivery.aspx. Imechukuliwa 06.06.2020

  8. NCBI. When and where to puch. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1804305/. Imechukuliwa 06.06.2020

  9. Pushing during labor more isint better. https://www.parents.com/pregnancy/giving-birth/labor-and-delivery/pushing-during-labor-more-isnt-better/. Imechukuliwa 06.06.2020

bottom of page