top of page

Mwandishi:

Dkt. Adolf S, MD

Mhariri:

Dkt. Sospeter M, MD

1 Septemba 2022 18:25:08

Image-empty-state.png

Wiki ya 36 ya ujauzito


Viungo vyote vya mtoto huwa vimekoma na mtoto huweza kuishi nje ya mwili wa mama, mama anaweza kupata uchungu muda wowote ule.


Nini hutokea kwa mtoto


 • Kwa sehemu kubwa mifumo na ogani za mwili wake huwa zimekomaa kumuwezesha kuishi nje ya tumbo la uzazi, hata hivyo mtoto anayezaliwa kipindi hiki bado huhesabika kama njiti

 • Uzito wake hufikia takribani gramu 2700


Nini hutokea kwa mama


 • Anaweza kupata uchungu muda wowote kuanzia mwishoni mwa wiki ya 36

 • Mama anaweza kupata msongo na wasiwasi kuhusu leba na malezi ya mtoto hasa ikiwa ni ujauzito wa kwanza

Nini cha kufanya


 • Kama ni ujauzito wa kwanza jifunze kuhusu dalili na viashiria vya uchungu

 • Fanya maandalizi ya kupokea mtoto kiakili, kifedha nk.

 • Pata sapoti kutoka kwa mwenza, marafiki, ndugu na watu walio karibu nawe. Hii itakusaidia kuondoa msongo na wasiwasi.


Majina mengine

Majina mengine yanayoendana na mada hii ni:

 • Ujauzito wa wiki 36

 • Mimba ya wiki 36

 • Wiki 36 ya mimba

 • Kijusi cha wiki 36

 • Mwonekano wa ujauzito wa wiki 36

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 19:33:03

Rejea za dawa

 1. American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]

 2. Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]

 3. Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]

 4. McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]

 5. Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]

 6. Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]

 7. Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]

 8. ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]

 9. Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]

bottom of page