top of page

Elimu ya magonjwa kwa mjamzito

Sehemu hii utajifunza maelezo ya ziada kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa ujauzito. Unashauriwa siku zote kuwasilaina na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile iliyoandikwa humu ili kupata ushauri unaoendana na hali yako ya kiafya.

Wiki ya 12 ya ujauzito

Wiki ya 12 ya ujauzito

Katika wiki hii umbo na sura halisi ya binadamu huonekana lakini masikio huwa hayajakua vizuri.
Ngozi ya mtoto huwa nyembamba kiasi cha kuonyesha vilivyomo ndani ya mwili wake kama vile mishipa ya damu.

Wiki ya 11 ya ujauzito

Wiki ya 11 ya ujauzito

Katika kipindi hiki, kijusi hukua na kupata taswira ya binadamu, licha ya kichwa chake kuwa cha mviringo huwa chenye mabonde na macho yake huwa yamefunikwa na kibugiko cha jicho.

Kichefuchefu na kutapika kwa mjamzito

Kichefuchefu na kutapika kwa mjamzito

Kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito hutokea sana katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito na dalili kupotea kuanzia wiki ya 22, hata hivyo asilimia 10 ya wanawake huwa na dalili endelevu hadi wakati wa kujifungua.

Kisukari kwa mjamzito

Kisukari kwa mjamzito

Kisukari ni ugonjwa sugu usiombukiza unaosababishwa na kuathirika kwa mfumo unaohusika na uchakatwaji na utumiaji ya sukari yaani glukosi katika mwili kutokana na kushindwa kuzalishwa au kufanya kazi kwa homoni ya insulin.

Sonona kwa mjamzito

Sonona kwa mjamzito

Japo ni kawaida kwa binadamu kupata huzuni katika vipindi tofauti vya maisha, mjamzito atasemekana kuwa na sonona kama akipata hali hii kwa muda wa wiki 2 au zaidi na kuambatana na dalili kama vile kukosa hamu ya kula, kupungua uzito, kukosa usingizi.

bottom of page