top of page

Elimu ya magonjwa kwa mjamzito

Sehemu hii utajifunza maelezo ya ziada kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa ujauzito. Unashauriwa siku zote kuwasilaina na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile iliyoandikwa humu ili kupata ushauri unaoendana na hali yako ya kiafya.

Rhesus na ujauzito

Rhesus na ujauzito

Ugonjwa wa rhesus husababisha kuharibika kwa ujauzito zinazofuata baada ya ujauzito wa kwanza. Hutokea kwa mama mwenye rhesus hasi aliyebeba mtoto mwenye damu ya rhesus chanya aliyorithi kwa baba yake.

Maandalizi ya kubeba mimba

Maandalizi ya kubeba mimba

Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa, kubeba ujauzito baada ya kufanya maandalizi huambatana na matokeo mazuri ya ujauzito.

Mjamzito kuvimba miguu

Mjamzito kuvimba miguu

Ni hali ya kawaida kutokea kwenye kanyagio hadi usawa wa kifundo cha mguu na huzidi sana kipindi cha tatu cha ujauzito. Endapo utatokea kwa haraka, kwenye mguu mmoja au kuwa na maumivu, wasiliana na daktari haraka kwa uchunguzi na tiba.

Leba kabla ya wakati

Leba kabla ya wakati

Leba kabla ya wakati hutokea mama anapopata uchungu na kufunguka kwa shingo ya kizazi muda wowote baada ya ujauzito kutimiza wiki 28 na kabla ya wiki 37. Wasiliana na daktari haraka ukipata dalili za hatari kipindi hiki.

Mtoto njiti

Mtoto njiti

Mtoto njiti ni mtoto aliyezaliwa hai kabla ya ujauzito kutimiza wiki 37 kamili, kwa sababu mtoto njiti huzaliwa kabla ya kukomaa vema, huwa na hatari kubwa ya kupata maradhi, madhaifu ya ukuaji na kifo. Kupata huduma sahihi na kushirikiana na daktari hupunguza madhara na kuongeza uwezekano wa kuishi.

bottom of page