top of page

Elimu ya magonjwa kwa mjamzito

Sehemu hii utajifunza maelezo ya ziada kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa ujauzito. Unashauriwa siku zote kuwasilaina na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile iliyoandikwa humu ili kupata ushauri unaoendana na hali yako ya kiafya.

Ethionamide na ujauzito

Ethionamide na ujauzito

Ingawa tafiti za wanyama zinaonyesha kuwepo na hatari ya kutokea madhaifu ya kimaumbile kwa watoto wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii , taarifa za binadamu zinapendekeza kuwa hatari iliyopo ni kidogo na endapo imependekezwa tumika, isisitishwe kutumika kwa sababu ya ujauzito.

Chloramphenicol na ujauzito

Chloramphenicol na ujauzito

Ingawa ya kuwa si sumu kwa kichanga, chloramphenicol inapaswa kutumika kwa tahadhari. Ripoti moja ilidai kwamba watoto wanaozaliwa na wamama waliotumia dawa hii katika kipindi cha kwanza cha ujauzito walikuwa wanapata gray syndrome. Ripoti za ziada bado hazijapatikana, hata hivyo inafahamika vema kuwa, vichanga wanaotumia dawa hii kwa dozi kubwa huweza kupata gray syndrome. Kwa sababu hii, baadhi ya watafiti wanashauri dawa hii isiwe kwenye kundi la dawa zinazopatana na ujauzito.

Azithromycin na ujauzito

Azithromycin na ujauzito

Azithromycin, ni dawa ya azalide inayotokana na erythromycin. Dawa hii ipo kundi la dawa zinazoitwa
macrolide ikijumuisha clarithromycin na erythromycin. Taarifa za ujauzito wa binadamu, hauonyeshi kuwa dawa hii inasababisha madhara ya kiuumbaji kwa mtoto.

Ondansetron  na ujauzito

Ondansetron na ujauzito

Taarifa nyingi za wanyama na binadamu zinaonyesha kuwa dawa hii ina hatari kidogo ya kusababisha ulemavu kwa vichanga watakaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii.

Efavirenz na ujauzito

Efavirenz na ujauzito

Taarifa za binadamu zipo chache sana kuruhusu kutabiri kuhusu hatari kwa kijusi tumboni na madhaifu ya kiuumbaji itakapotumika wakati wa ujauzito. Madhara ya kiuumbaji yaliyoonekana kwa nyani na panya inatoa ushuhuda kuwa na uwezekano mkubwa wa hatari kwa binadamu. Dawa hii huweza kupita kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na hivyo kuongezeka kwa hatari ya mtoto. Ripoti ya nyani ilionyesha kutokea kwa mgongo wazi (myelomeningocele) kutokana na matumizi ya dawa hii. Kwa ujumla wake, taarifa bado hazitoi majibu moja kwa moja kwamba efavirenz ni sumu kwa kichanga wa binadamu na hivyo isisitishwe kwa endapo ni muhimu kutumika kwa mama mjamzito.

bottom of page