top of page

Elimu ya magonjwa kwa mjamzito

Sehemu hii utajifunza maelezo ya ziada kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa ujauzito. Unashauriwa siku zote kuwasilaina na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile iliyoandikwa humu ili kupata ushauri unaoendana na hali yako ya kiafya.

Adefovir na ujauzito

Adefovir na ujauzito

Ni dawa ya kutibu maambukizi ya virusi ilio ambayo inafanana na adenosine monophosphate.Taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo kwa hatari kidogo,licha ya taarifa za binadamu kuwa chache. Endapo itapendekezwa kutumika kwenye matibabu, inatakiwa isisitishwe kutumika kwa sababu ya ujauzito.

Cetirizine kwa mjamzito

Cetirizine kwa mjamzito

Cetirizine hausababishi ulemavu kwa watoto wa wanyama wajawazito waliopewa dawa hii, hata hivyo hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha usalama wa dawa hii kwa binadamu.

Itraconazole na ujauzito

Itraconazole na ujauzito

Itraconazole ni dawa ya kutibu fangasi jamii ya triazole. Uzoefu wa matumizi ya dawa hii kwenye ujauzito unaonyesha kuwepo kwa hatari kidogo sana ya madhaifu ya kiuumbaji kwa vichanga wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii wakati wa ujauzito. Hata hivyo dawa zingine za triazole fluconazole, imeonyesha mahusiano kusababisha madhaifu ya kimaumbile kwa mtoto, mahusiano hayo yanahisiwa kuhusiana na dozi iliyotumika. Kwa dawa ya itraconazole, taarifa za wanyama haziwezi kujitosheleza kutafsiri kuwa sumu kwa binadamu mjamzito. Hivyo ni vema dawa hii ikazuiwa kipindi cha kwanza cha ujauzito kama ikiwezekana. Endapo matumizi ya dawa hii ni lazima kwenye kipindi cha kwanza cha ujauzito, mama anatakiwa ashauriwe kuwa hatari ya madhaifu kwa kichanga ni ndogo san ahata kama yapo.

Thiamine na ujauzito

Thiamine na ujauzito

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa thiamine ni salama wakati wa ujauzito endapo itatumika katika dozi inayoruhusiwa kutumika katika ujauzito.

Cefuroxime na ujauzito

Cefuroxime na ujauzito

Tafiti kwenye panya zimeonyesha dawa haina madhara kwenye uzazi kwenye dozi iliyotumika ambayo ni sawa na mara 9 ya dozi inayotakiwa kutumika kwa binadamu, panya, na nyani.

bottom of page