top of page

Elimu ya magonjwa kwa mjamzito

Sehemu hii utajifunza maelezo ya ziada kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa ujauzito. Unashauriwa siku zote kuwasilaina na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile iliyoandikwa humu ili kupata ushauri unaoendana na hali yako ya kiafya.

Amoxiclavu na ujauzito

Amoxiclavu na ujauzito

Tafiti nyingi zimeonyesha kutokuwepo kwa madhara kwa kijusi na mtoto anayezaliwa. Hata hivyo tafiti moja imeripoti kuwa kuna mahusiano kati ya matumizi ya dawa hii na kutokea kwa ugonjwa wa kuoza kwa utumbo wa mtoto kwa vichanga wanaozaliwa.

Metoclopramide na ujauzito

Metoclopramide na ujauzito

Hutumika kwenye vipindi vyote vitatu vya ujauzito kuzuia kichefuchefu na kutapika. Taarifa za tafiti kuhusu kusababisha ulemavu kwa kichanga zinakinzana hata hivyo tafiti nyingi zinaonyesha kuwa ni salama katika kipindi chochote kile cha ujauzito.

Rifabutin na ujauzito

Rifabutin na ujauzito

Hakuna taariza inayoelezea matumizi ya rifabutin kwa binadamu wajawazito, taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo na hatari kidogo ya kupata madhaifu ya kiuumbaji wa watoto wanaozaliwa na wanyama wajawazito waliotumia dawa hii. Hata hivyo, licha ya hatari hiyo kwa wanyama, faida za matumizi kwa binadamu ni kubwa kuliko madhara yanayoweza kujitokeza. Inapoanzishwa haitakiwi kuacha tumika kwa sababu ya ujauzito.

Ciprofloxacin kwa mjamzito

Ciprofloxacin kwa mjamzito

Matumizi ya ciprofloxacin kipindi cha kwanza cha ujauzito yaani wiki 12 za mwanzoni huwa na uhusiano wa moja kwa moja wa kusababisha ulemavu kwa vichanga. Baadhi ya tafiti na wataalamu wa afya wanashauri kutotumia kabisa dawa hii wakati wa ujauzito.

Kanamycin na ujauzito

Kanamycin na ujauzito

Dawa hiii imeripotiwa kuwa sumu kwenye masikio, hata hivyo hakuna ripoti ya kusababisha madhaifu mengine ya kiumbaji ya maungo mbalimbali ya mwili kwa watoto wanaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii katika kipindi cha kwanza cha ujauzito.

bottom of page