top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. peter R, CO

Dkt. Benjamin L, MD

Alhamisi, 18 Novemba 2021

Asparagus
Asparagus

Asparagus mmea wenye asili ya Ulaya, huvunwa na kutumika kama chakula kikiwa bado halijakomaa. Licha ya kuwa na mwonekano wake wa kustaajabisha, asparagus huwa viinilishe na virutubisho vya kutosha, ndio maaana umeenea duniani kote. Unaweza kupata mmea huu kwenye masoko makubwa na makuda pia.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Asparagus


  • Sukari

  • Mafuta

  • Nyuzilishe

  • Protini

  • Vitamini

  • Madini

  • Kabohaidreti


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Asparagus yenye gramu 100


  • Nishati = 85kcal

  • Sukari = 1.88g

  • Nyuzilishe = 2.1g

  • Mafuta = 0.12g

  • Protini = 2.2g


Madini yanayopatikana kwenye Asparagus yenye gramu 100


  • Kalishiamu = 24mg

  • Madini Chuma = 2.14mg

  • Magineziamu = 14mg

  • Manganaizi = 0.158mg

  • Fosifolasi = 52mg

  • Potashiamu = 202mg

  • Sodiamu = 2mg

  • Zinki = 0.54mg


Vitamini zinazopatikana kwenye Asparagus yenye gramu 100


  • Vitamini A = 38mcg

  • Vitamini B1 = 0.143mg

  • Vitamini B2 = 0.141mg

  • Vitamini B3 = 0.978mg

  • Vitamini B5 = 0.274mg

  • Vitamini B6 = 0.091mg

  • VItamini B9 = 52mcg

  • Vitamini C = 5.6mg

  • Vitamini E = 1.1mg

  • Vitamini K = 41.6mcg


Faida za kiafya zitokanazo na utumiaji wa asparagus




  • Kuimarisha mifupa

  • Inongeza uwezo wa kuishi muda mrefu (inapunguza kasi ya kuzeeka)

  • Kuimarisha mishipa ya damu na kuzuia shinikizo la juu la damu

  • Kuimarisha afya ya moyo na kupunguza hatari ya kupata shambulio la moyo

  • Kuimarisha mfumo mzima wa mmeng`enyo wa chakula

  • Kusaidia maendeleo na ukuaji wa motto aliye tumboni kwa wajawazito

  • Kuimarisha kinga ya mwili

  • Kuasaidia kupunguza uzito usiotakiwa mwilini


Imeboreshwa,
18 Novemba 2021 07:37:13
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. In the eleventh century AD the word "asparagus" appeared in an English text. See Brunning (June 2010), p. 6.

  2. Plants of the World Online. (n.d.). "Asparagus officinalis L." Royal Botanic Gardens, Kew. Imepitiwa tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka 2021

  3. Murphy, Andrew R. (8 October 2018). William Penn: A Life. Oxford University Press. ISBN 978-0-19-023426-3.

bottom of page