Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter A,MD
Dkt. Mangwella S, MD
Jumamosi, 4 Desemba 2021
Beri ya bluu
Beri ya bluu ni zao la mimea linalopatikana kwenye kundi mizabibu, tunda hili linataka kufanana na tunda la zabibu. Kuanzia rangi mpaka umbile ijapokuwa tofauti yake ni kidogo sana hasa kwenye umbile. Tunda hili linalimwa sana nchi ya amerika ya kaskazini kasha kutapaa duniani kote na linapatikana kwa wingi kwenye masoko na supamaketi mabalimabali hapa nchini kwetu Tanzania.
Kama ilivyo kwa mtunda matunda mengine, Beri ya Bluu pia inafaida kwa afya na ni salama kwa matumizi ya Binadamu kwani huwa na virutubisho na vitamini kwa kuboresha afya ya mwanadamu. Inawezatumika kama juisi, kuitafuna ikiwa mbichi, kuchanganya kwenye vyakula (inashauriwa kutumika kama juisi au kutumia ikiwa mbichi).
Viinilishe vinavyopatikana kwenye beri ya bluu
Nishati
Protini
Mafuta
Sukari
Nyuzilishe
Maji
Kabohaidreti
Vitamini
Madini
Viinilishe vinavyopatikana kwenye beri ya bluu zenye gramu 100
Nishati = 57kcal
Protini = 0.7g
Nyuzilishe = 2.4g
Mafuta = 0.3g
Sukari =10g
Maji = 84.21g
Kabohaidreti = 14g
Madini yanayopatikana kwenye beri ya bluu yenye gramu 100
Kalishiamu = 6mg
Madini Chuma = 0.28mg
Magineziamu = 6mg
Kopa = 0.057mg
Manganaizi = 0.336mg
Fosifolasi = 12mg
Potashiamu = 77mg
Sodiamu = 1mg
Zinki = 0.16mg
Vitamini zinazopatikana kwenye beri ya bluu yenye gramu 100
Vitamini A = 3mcg
Karotini Bita = 32mcg
Vitamini B1 =0.37mcg
Vitamini B2 = 0.041mcg
Vitamini B3 = 0.418mcg
Vitamini B5 = 0.124mcg
Vitamini B6 = 0.052mcg
Vitamini B9 = 6mcg
Vitamini C = 9.7mcg
Vitamini E = 0.57mcg
Vitamini K = 19.3mcg
Faida za beri ya bluu
Beri ya bluu huwa na faida zifuatazo;
Kuimarisha afya ya mifupa na ngozi
Kupunguza kasi ya kupata athari ya kansa
Inasaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini, pia inashauriwa kutumiwa na wagonjwa wa sukari
Kurekebisha shinikizo la juu la damu
Kuboresha afya ya akili
Kuimarisha kinga ya mwili
Imeboreshwa,
4 Desemba 2021 14:08:35
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Devore E, Kang HJ, Breteler MM, Grodstein F. Dietary intakes of berries and flavonoids in relation to cognitive decline. Ann Neurol. 2012;72:135–43.
Williamson G, Clifford MN. Colonic metabolites of berry polyphenols: the missing link to biological activity?. Br J Nutr. 2010;104:S48–66.
Cassidy A, O'Reilly EJ, Kay C, Sampson L, Franz M, Forman JP, Curhan G, Rimm EB. Habitual intake of flavonoid subclasses and incident hypertension in adults. Am J Clin Nutr. 2011;93:338–47.
https://uc.xyz/14f3Oq?pub=link [Recent Research on the Health Benefits of Blueberries and Their Anthocyanins - PubMed]. Imechukuliwa 30/11/2021.