top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, CO

Dkt. Mangwella S, MD

Jumatatu, 21 Machi 2022

Bilinganya
Bilinganya

Bilinganya ni zao linalopatikana kwenye familia ya Solanaceae, ambapo hutumika kama mboga baada ya kupikwa ili kuliwa kama chakula.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Bilinganya


 • Mafuta

 • Madini

 • Sukari

 • Nyuzilishe

 • Protini

 • Vitamini

 • Kabohaidreti

 • Maji


Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Bilinganya


Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Bilinganya ni Acetylcholine.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Biliganya yenye gramu 100


 • Nishati = 25kcal

 • Mafuta = 0.2g

 • Maji = 92.3g

 • Kabohaidreti = 5.9g

 • Sukari = 3.5g

 • Nyuzilishe = 3g

 • Protini = 1g


Vitamini zinazopatikana kwenye Bilinganya yenye gramu 100


 • Vitamini A = 1mcg

 • Vitamini B1 = 0.039mg

 • Vitamini B2 = 0.037mg

 • Vitamini B3 = 0.649mg

 • Viatmini B5 = 0.281mg

 • Viatmini B6 = 0.084mg

 • Vitamini B9 = 22mcg

 • Vitamini C =2.2mg

 • Vitamini E =0.3mg

 • Vitamini K = 3.5mg


Madini yanayopatikana kwenye Bilinganya yenye gramu 100


 • Kalishiamu = 9mg

 • Kopa = 0.8mg

 • Madini Chuma = 0.23mg

 • Magineziamu = 14mg

 • Manganaizi = 0.232mg

 • Fosifolasi = 24mg

 • Potashiamu = 229mg

 • Sodiamu = 2mg

 • Zinki = 0.16mg


Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Bilinganya


 • Kulinda na kuimarisha seli hai nyeupe mwilini.

 • Kupunguza uzito mwilini

 • Kupunguza athari za kupatwa na magonjwa ya moyo Pamoja na ugonjwa wa shinikizo la juu la Damu.

 • Kuweka msawazo wa suakri mwilini na kupunguza athari za kupatwa na ugonjwa wa kisukari

 • Kuuikinga mwili dhidi ya kansa za aina mbalimabali


Imeboreshwa,
21 Machi 2022 11:44:20
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

bottom of page