Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Sospeter M, MD
Jumatatu, 21 Machi 2022
Boga
Boga ni tunda la msimu lenye rangi za aina mbalimbali kutoka kundi la Cucurbitaceae. Tunda hili ni maarufu katika afya kutokana na kushamiri virutubisho na madini mbalimbali.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Boga
Mafuta
Madini
Sukari
Nyuzilishe
Protini
Vitamini
Kabohaidreti
Maji
Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Boga
Boga lina kemikali muhimu ziitwazo Linoleic Acid, Oleic Acid Pamoja na Amino Acid.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Boga lenye gramu 100
Nishati = 26kcal
Mafuta = 01g
Maji = 91.6g
Kabohaidreti = 6.5g
Sukari = 2.8g
Nyuzilishe = 0.5g
Protini = 1g
Vitamini zinazopatikana kwenye Boga lenye gramu 100
Vitamini A = 426mcg
Vitamini B1 = 0.05mg
Vitamini B2 = 0.110mg
Vitamini B3 = 0.6mg
Viatmini B5 = 0.298mg
Vitamini B6 = 0.061mg
Vitamini B9 = 16mcg
Vitamini C = 9mg
Vitamini E =1.06mg
Vitamini K = 1.1mg
Madini yanayopatikana kwenye Boga lenye gramu 100
Kalishiamu = 21mg
Kopa = 0.13mg
Madini Chuma = 0.8mg
Magineziamu = 12mg
Manganaizi = 0.125mg
Fosifolasi = 44mg
Potashiamu = 340mg
Sodiamu = 1mg
Zinki = 0.32mg
Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Maboga
Huimarisha afya ya uzazi kwa wanaume
HUimarisha na kuboresha afya ya moyo na kuzuia shinikizo la juu la Damu
Huweka usawa baina ya uwiano uzito na urefu
Huongeza uwezo wa kuona na kuimarisha afya ya macho.
Husawazishasukari kwenye damu
Huimarisha na kuongeza kinga ya mwili
Huzuia athari za kupatwa na saratani za aina mbalimbali.
Kuimarisha afya ya ngozi na kuifanya kuwa angavu.
Imeboreshwa,
21 Machi 2022 13:32:52
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Pumpkin. https://www.nutritionvalue.org/Pumpkin%2C_raw_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 13 January 2022.
Różyło R, Gawlik-Dziki U, Dziki D, Jakubczyk A, Karaś M, Różyło K. Wheat Bread with Pumpkin (Cucurbita maxima L.) Pulp as a Functional Food Product. Food Technol Biotechnol. 2014 Dec;52(4):430-438. doi: 10.17113/ftb.52.04.14.3587. PMID: 27904316; PMCID: PMC5079154. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/27904316/. Imechukuliwa tarehe 13 January 2022.
Adams G.G., Imran S., Wang S., Mohammad A., Kok S., Gray D.A., Channell G.A., Morris G.A., Harding S.E. The hypoglycemic effect of pumpkins as anti-diabetic and functional medicines. Food Res. Int. 2011;44:862–867. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6819838/. Imechukuliwa tarehe 13 January 2022.