Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter A, MD
Dkt. Mangwella S, MD
Jumatatu, 21 Machi 2022
Brokoli
Brokoli ni mimea ya kijani inayopotaikana kundi moja na kabichi (Brassica) na huliwa kama mboga. Mmea huu huwa na kiwango kikubwa vitamin C.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Brokoli
Mafuta
Madini
Sukari
Nyuzilishe
Protini
Vitamini
Kabohaidreti
Maji
Kemikali muhimu zinazopatikana kwenye Brokoli
Kemikali muhimu zinazopatikana kwenye Brokoli ni Lutein na zeaxanthin
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Brokoli yenye gramu 100
Nishati = 34kcal
Mafuta = 0.4g
Maji = 89.30g
Kabohaidreti = 6.6g
Sukari = 1.7g
Nyuzilishe = 2.6g
Protini = 2.8g
Vitamini zinazopatikana kwenye Brokoli yenye gramu 100
Vitamini A = 31mcg
Vitamini B1 = 0.071mg
Vitamini B2 = 0.117mg
Vitamini B3 = 0.639mg
Viatmini B5 = 0.573mg
Vitamini B6 = 0.175mg
Vitamini B9 = 63mcg
Vitamini C = 89.2mg
Vitamini E =0.78mg
Vitamini K = 101.6mg
Madini yanayopatikana kwenye Brokoli yenye gramu 100
Kalishiamu = 47mg
Kopa = 0.05mg
Madini Chuma = 0.73mg
Magineziamu = 21mg
Manganaizi = 0.210mg
Fosifolasi = 66mg
Potashiamu = 316mg
Sodiamu = 33mg
Zinki = 0.41mg
Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Brokoli
Kuboresha afya ya macho na kuongeza uwezo wa kuona, na kuimarisha Ngozi kwa kuzuia athari zitokanazo na miale ya jua.
Kusaidia kuimarisha kinga ya mwili na mifupa. Pia inasaidia ukuaji wa mtoto tumboni (Mama mjamzito)
Kusaidia kuzuia athari zitokanazo na kansa za aina mbalimbali mfano kansa ya matiti, kansa ya tezi dume, kansa ya kibofu, kansa ya utumbo, na kansa ya figo.
Kuweka msawazo wa kiwango cha sukari kwenye damu, na kuzuia ugonjwa wa kisukari ule wa aina ya pili
Kusaidia kuimarisha afya ya moyo na kuondoa Rehemu kwenye mishipa ya damu.
Kusaidia mfumo wa mmeng`enyo wa chakula hivyo kuzuia tatizo la kupata choo kigumu.
Kuimarisha mfumo wa fahamu hasa hasa kwenye ubongo hivyo kusaidia kupunguza tatizo la kusahau na baadhi ya magonjwa yanayoshambulia ubongo.
Kusaidia kupunguza kasi ya kuzeeka Pamoja na kuimarisha afya ya kinywa na meno
Imeboreshwa,
21 Machi 2022 15:43:33
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Brococoli. https://www.nutritionvalue.org/Broccoli%2C_raw_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 2 February 2022.
Latté KP, Appel KE, Lampen A. Health benefits and possible risks of broccoli - an overview. Food Chem Toxicol. 2011 Dec;49(12):3287-309. doi: 10.1016/j.fct.2011.08.019. Epub 2011 Aug 28. PMID: 21906651. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/21906651/. Imechukuliwa tarehe 2 February 2022.
Vasanthi HR, Mukherjee S, Das DK. Retraction Notice To: Potential Health Benefits of Broccoli- A Chemico-Biological Overview. Mini Rev Med Chem. 2009 Jun;9(6):749-59. doi: 10.2174/138955709788452685. PMID: 19519500. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/19519500/. Imechukuliwa tarehe 2 February 2022.
Antioxidant and Anti-inflammatory Activities of Broccoli Florets in LPS-stimulated RAW 264.7 Cells written by Joon-Ho Hwang and Sang-Bin Lim. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4103733/. Imechukuliwa tarehe 2 February 2022.