Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Sospeter M, MD
Jumamosi, 4 Desemba 2021
Choya
Choya au rozela ni maua mekundu yaliyo kwenye familia ya mimea inayofahamika kama Malvakee na huwa na asili ya bara la Afrika hasa Afrika ya Kati licha ya sasa kusambaa barani Asia na kwa sasa inapatikana duniani kote. Maua ya choya huweza kutumika yakiwa mabichi au yamekaushwa na huwa na umuhimu mkubwa kutokana na virutubishi vilivyondani yake kama vilivyoelezewa kwenye makala hi.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye choya
Mafuta
Vitamini
Madini
Kabohaidreti
Protini
Maji
Viinilishe vinavyopatikana kwenye choya yenye gramu 100
Nishati = 49kcal
Protini = 1g
Kabohaidreti = 11g
Mafuta = 0.6g
Maji = 86.6g
Vitamini zinazopatikana kwenye choya yenye gramu 100
Vitamini A = 14mcg
Vitamini B1 = 0.011mg
Vitamini B2 = 0.03mg
Vitamini B3 = 0.03mg
Vitamini C = 12mg
Madini yanayopatikana kwenye choya yenye gramu 100
Kalishiamu = 215mg
Madini Chuma = 1.5mg
Magineziamu = 51mg
Fosifolasi = 37mg
Potashiamu = 208mg
Sodiamu = 6mg
Faida za choya
Faida za kiafya za choya ni;
Kupunguza maumivu ya tumbo kwa wanawake wanaokuwa kwenye hedhi
Kusaidia kwenye mmeng`enyo wa chakula
Kuongeza kinga ya mwili
Kupunguza na kurekebisha uzito usiotakiwa
Inasaidia kupambana na sonona
Inapunguza athari ya kupatwa na kansa
Inasaidia kulainisha koo na kupunguza homa (kwa wagonjwa)
Kurekebisha shinikizo la juu la juu la damu
Kuimarisha na kuimarisha mfumo mzima wa Ini
Kuimarisha na kuboresha afya ya Meno
Imeboreshwa,
4 Desemba 2021 15:02:15
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Yusni I., Syahrul M. Blood pressure reduction by rosela (Hisbiscus sabdariffa) in elderly women: role of vasodilation response of nitric oxide. Jurnal Kardiologi Indonesia. 2012;33(3):137–145.
Andraini T., Yolanda S. Prevention of insulin resistance with Hibiscus sabdariffa Linn. extract in high-fructose fed rat. Med J Indones. 2014;23(4):192–196.
Sansbury B. E., Hill B. G. Regulation of obesity and insulin resistance by nitric oxide. Free Radical Biology and Medicine. 2014;73:383–399.
Barhe T. A., Tchouya G. R. F. Comparative study of the anti-oxidant activity of the total polyphenols extracted from Hibiscus Sabdariffa L., Glycine max L. Merr., yellow tea and red wine through reaction with DPPH free radicals. Arabian Journal of Chemistry. 2016;9(1):1–8.