Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, C.O
Dkt. Sospeter M, M.D
Jumamosi, 22 Januari 2022
Duriani
Duriani ni tunda lenye kufanana na stafeli kwa umbile, linalopatikana kwenye kundi la durii kutoka kwenye familia ya Malvaceae.
Tunda hili huwa kubwa, lenye ganda gumu kwa nje na huwa na harufu kali ijapokuwa lina ladha tamu.
Viinirishe vinavyopatikana kwenye tunda la Duriani
Mafuta
Kabohaidreti
Nyuzilishe
Protini
Madini
Vitamini
Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Duriani
Kwenye Tunda la Duriani tunapata kemikali ambazo ni Stearic Acid, Palmit Acid na Palmitolec Acid
Viinirishe vinavyopatikana kwenye tunda la Duriani
Nishati= 147kcl
Jumla ya mafuta = 5.33g
Kabohaidreti = 27.1g
Maji = 65g
Nyuzilishe = 3.8g
Protini = 1.47g
Madini yanayopatikana kwenye Tunda la Duriani lenye Gramu 100
Madini chuma = 0.43mg
Kalishiamu = 6mg
Magineziamu = 30mg
Fosifolasi = 39mg
Potashiamu = 436mg
Sodiamu = 2mg
Manganaizi = 0.325mg
Koppa = 0.207mg
Zinki = 0.28mg
Vitamini zinazopatikana kwenye Tunda la Duriani lenye gramu 100
Vitamin A = 3mcg
Vitamini B1 = 0.017mg
Vitamini B2 = 0.026mg
Vitamini B3 = 0.091mg
Vitamini B5 = 0.061mg
Vitamini B6 =0.041mg
Vitamini B9 = 3mcg
Vitamini C = 4.6mg
Vitamini E = 0.18mg
Vitamini K = 2.2mcg
Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa tunda la Duriani
Kupunguza athari za kupatwa na ugonjwa Wa Kansa za aina mbalimbali.
Kuzuia magonjwa ya moyo kuzuia shinikizo La juu la Damu pamoja na kurekebisha mishipa ya Damu.
Kuimarisha kinga ya mwili.
Kurekebisha na kupunguza kiwango cha sukari mwilini
Kupunguza joto la mwili (kwa wagonjwa)
Kuimarisha na Kutibu magonjwa ya ngozi
Imeboreshwa,
22 Januari 2022 17:23:00
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Ho LH, Bhat R. Exploring the potential nutraceutical values of durian (Durio zibethinus L.) - an exotic tropical fruit. Food Chem. 2015 Feb 1;168:80-9. doi: 10.1016/j.foodchem.2014.07.020. Epub 2014 Jul 11. PMID: 25172686.
Brown MJ, Durio-A Bibliographic Review (International Plant Genetic Resources Institute. IPGRI office for South Asia, New Delhi) 1997.
Durian nutritional value. https://www.nutritionvalue.org/Durian%2C_raw_or_frozen_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 28 December 2021