top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

3 Aprili 2026, 04:13:29

Faida za kiafya za mbegu ya tikiti
Faida za kiafya za mbegu ya tikiti

Utangulizi: Kwa nini usidharau mbegu za tikiti?

Kuna vitu ambavyo umekuwa ukividharau au kuona havifai kabisa unapokuwa unakula vyakula aina fulani haswa ikija kwenye ulaji wa mbegu au maganda ya matunda kama zabibu, maboga n.k. Kusoma makala hii itakusaidia kufahamu kiundani kuhusu faida za kiafya za mbegu za tikiti maji na namna ya kutumia mbegu hizo ili kupata faida zake.


Kwanza kabisa ufahamu kuwa mbegu za tikiti ni miongoni mwa mbegu ambazo zina virutubisho kwa wingi sana zaidi ya unavyofikiria. Mbegu hizi pamoja na mbegu za maboga zimekuwa zikitumika kwa matumizi mbalimbali vijijini. Mfano watu walipokuwa wanaandaa mrenda mkavu hutumia karanga za maboga kasha kuzitwanga kwa pamoja mpaka zikawa unga kasha kupikwa. Chakula hiki huwa kitamu sana na ndio maana watu wa zamani waliokuwa wanatumia vyakula hivi walikuwa wanaishi miaka mingi bila kuwa na magonjwa kama yalivyo kipindi cha sasa cha karne ya 20.


Virutubisho Vilivyomo Ndani ya Mbegu za Tikiti Maji

Mbegu za tikiti zina virutubisho vifuatavyo kwa wingi:

  • Protini

  • Vitamin

  • Mafuta ya omega-3

  • Madini ya magnesium

  • Zinki

  • Madini shaba

  • Madini chuma

  • Madini ya potassium

  • Na vingine vingi


Faida za mbegu za tikiti maji mwilini


Faida kwa Ngozi

Endapo utatumia kwa mpangilio mbegu za tikiti utapata faida halisi za mbegu ambazo ni:

  • Kutosumbuliwa na chunusi mwilini

  • Ngozi yako kuwa laini na kutopata shida ya ngozi kupasuka pasuka

  • Ngozi yako haitakunjamana mapema (haitazeeka mapema)

Kumbuka unaweza kutumia mafuta ya mbegu hizi kupaka kwenye ngozi ili kuzuia chunusi kuota.


Faida kwa Nywele

Nywele huhitaji madini chuma, protini na shaba ili kuweza kuwa imara na kukua vema. Endapo utapaka mafuta ya tikiti kwa kipindi kirefu nywele zako zitapata faida zifuatazo:

  • Kuondokana na nywele kunyonyoka

  • Nywele kuwa nzito na nyingi

  • Kuacha kukatika

  • Kupata rangi nzuri na iliyokolea zaidi


Kuongeza Nguvu Mwilini

Kwa sababu mbegu za tikiti maji huwa na nishati kwa wingi zinazotoka kwenye mafuta yake ya omega 3, ukitumia kikombe kimoja cha mbegu hizi utapata faida zifuatazo:

  • Mwili kuimarika kwa kupata nguvu na virutubisho muhimu

  • Kuongezeka uzito endapo zitatumika kwa wingi zaidi


Kuimarisha Afya ya Mifupa

Endapo utatumia mbegu za tikiti maji kwa muda mrefu utapata faida zifuatazo:

  • Kujikinga na tatizo la osteoporosis (udhaifu wa mifupa unaohusiana na uzee)

  • Mifupa kuwa imara zaidi katika maisha yote


Jinsi ya kupata faida hii

Ukitumia kikombe kimoja cha chai utapata zaidi ya kiwango kinachohitajika kwa siku, pamoja na madini mengine muhimu kwa afya ya mifupa.


Kudhibiti Kiwango cha Sukari Kwenye Damu

Endapo utatumia mbegu za tikiti kwa muda mrefu utapata faida zifuatazo:

  • Mwili kudhibiti kiwango cha sukari

  • Kongosho kuzalisha vizuri homoni ya insulin

  • Kupunguza upinzani wa insulin

Endapo mgonjwa wa kisukari atatumia mbegu hizi kwa muda mrefu, anaweza kuona mwili ukianza kudhibiti sukari vizuri hivyo kupunguza utegemezi wa dozi kubwa za dawa.

Kwa watu wasiokuwa na kisukari, matumizi ya mbegu hizi yanaweza kusaidia kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.


Kuongeza Kiwango cha Shahawa

Kwa sababu huwa na madini ya zinki kwa wingi, mbegu hizi huongeza uzalishaji wa shahawa. Matumizi ya mara kwa mara yanaweza kusaidia kuboresha uwezo wa uzazi.


Kuongeza Kinga ya Mwili

Kutokana na kuwa na madini chuma na vitamin B, mbegu hizi zina uwezo wa kuongeza kinga za mwili endapo zitatumika kwa muda mrefu.


Namna ya kutumia mbegu za tikiti ili kupata faida zake

  • Tengeneza juisi ya tikiti na ndizi kwa kuiblendi na kunywa bila kuchuja

    Unaweza kuchanganya vipande vya tikiti maji pamoja na ndizi kisha kuviblendi bila kuchuja ili kuhakikisha mbegu zinaingia kwenye juisi. Njia hii husaidia kupata virutubisho vyote vilivyomo kwenye mbegu pamoja na matunda yenyewe, na ni nzuri kama kinywaji cha kuongeza nguvu mwilini hasa asubuhi.

  • Kausha mbegu za tikiti, kisha zikaange na kula kama karanga

    Baada ya kutoa mbegu kwenye tikiti, zikaushe vizuri juani au kwa hewa ya kawaida, kisha zikaange kwa joto la wastani bila mafuta mengi. Hii huboresha ladha na kufanya ziwe rahisi kuliwa kama vitafunwa (snack) vyenye afya ambavyo unaweza kutumia wakati wowote wa siku.

  • Changanya mbegu zilizokaangwa na milo mingine au kula peke yake

    Mbegu zilizokaangwa zinaweza kuongezwa kwenye vyakula mbalimbali kama wali, uji, saladi au hata maziwa mgando ili kuongeza thamani ya lishe ya mlo wako. Pia unaweza kuzila peke yake kama chakula cha haraka kati ya milo (kitafunwa) ili kuongeza nishati na virutubisho mwilini.


Maswali yaliyoulizwa mara kwa mara na majibu yake kuhusu mbegu za tikiti

1. Je, mbegu za tikiti zinaweza kuliwa zikiwa mbichi moja kwa moja?

Ndiyo, zinaweza kuliwa mbichi, lakini mara nyingi huwa ngumu kumeng’enywa vizuri na mwili. Kuzikausha au kuzikaanga kidogo husaidia kuboresha ladha na kufanya mwili uzitumie vizuri zaidi.

2. Je, mbegu za tikiti zinaweza kusaidia katika kupunguza uzito?

Zinaweza kusaidia kwa kiasi fulani ikiwa zitatumiwa kwa kiasi kidogo kama sehemu ya lishe yenye uwiano. Hutoa hisia ya kushiba na hivyo kupunguza ulaji wa vyakula vingine, lakini matumizi kupita kiasi yanaweza kuongeza kalori na kuathiri malengo ya kupunguza uzito.

3. Ni kiasi gani cha mbegu za tikiti kinachoshauriwa kwa siku?

Hakuna kiwango rasmi kilichowekwa, lakini kwa ujumla kiasi kidogo hadi cha wastani (kama kiganja kimoja hadi viwili kwa siku) kinatosha kupata faida bila kuongeza kalori kupita kiasi.

4. Je, mbegu za tikiti zinaweza kuharibika?

Ndiyo, zinaweza kuharibika hasa kutokana na mafuta yaliyomo ambayo yanaweza kuwa mabaya (rancid). Ni muhimu kuzihifadhi sehemu kavu, baridi na kwenye chombo kisichopitisha hewa.

5. Je, watoto wanaweza kutumia mbegu za tikiti?

Ndiyo, watoto wanaweza kuzitumia lakini kwa kiasi kidogo na zikiwa zimeandaliwa vizuri (kama kukaangwa au kusagwa) ili kuepuka hatari ya kukwama kooni.

6. Je, mbegu za tikiti zinaweza kusaidia afya ya akili?

Zinaweza kusaidia kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa kuwa na virutubisho vinavyohusika katika utendaji wa ubongo na usawazishaji wa kemikali za mwili zinazochangia utulivu wa akili.

7. Je, mbegu za tikiti zinaweza kuingiliana na dawa?

Kwa watu wanaotumia dawa za kudhibiti sukari au presha, ni vyema kuwa waangalifu kwani mbegu hizi zinaweza kusaidia kushusha viwango hivyo na kuongeza athari ya dawa. Ushauri wa daktari unapendekezwa.

8. Je, kuna tofauti kati ya mbegu za tikiti maji na mbegu za tikiti pori?

Ndiyo, kuna tofauti kidogo katika ukubwa, ladha na kiwango cha virutubisho, lakini kwa ujumla zote zina thamani ya lishe na zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiafya.

9. Je, mafuta ya mbegu za tikiti yanaweza kutumika vipi zaidi ya kula?

Mbali na matumizi ya chakula, mafuta haya yanaweza kutumika kwenye ngozi na nywele kama sehemu ya utunzaji wa mwili kutokana na sifa zake za kulainisha na kulinda.

10. Je, mbegu za tikiti zinafaa kwa watu wenye matatizo ya tumbo?

Zinaweza kuwa na manufaa kwa baadhi ya watu, lakini kwa wengine zinaweza kusababisha usumbufu kama gesi au kujaa tumbo, hasa zikiliwa kwa wingi. Ni vyema kuanza na kiasi kidogo na kuona mwitikio wa mwili.


Imeandikwa;
3 Aprili 2026, 04:13:29
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. Are Watermelon Seeds Healthy? Everything You Need To Know. https://www.ndtv.com/health/health-benefits-of-watermelon-seeds-are-watermelon-seeds-healthy-everything-you-need-to-know-1869355#. Imechukuliwa 25.11.2020

  2. Healthline. Health benefit of watermelon seeds. https://www.healthline.com/health/diabetes/watermelon-and-diabetes. Imechukuliwa 25.11.2020

  3. Amazing health benefits of eating watermelon seeds. https://timesofindia.indiatimes.com/life-style/food-news/wonder-health-benefits-of-ashwagandha/articleshow/68371805.cms. Imechukuliwa 25.11.2020

  4. 9 Magical Health Benefits Of Watermelon Seeds. https://pharmeasy.in/blog/9-magical-health-benefits-of-watermelon-seeds/. Imechukuliwa 25.11.2020

  5. Health benefit of watermelon seeds. https://www.femina.in/wellness/diet/benefits-of-watermelon-seeds-149318.html. Imechukuliwa 25.11.2020

bottom of page