Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Sima A, CO
Dkt. Mangwella S, MD
Jumanne, 5 Mei 2020
Faida za madini Shaba mwilini
Shaba ni moja ya madini yenye umuhimu sana mwilini, hupatikana katika tishu zote mwilini na hufanya kazi ya kutengeneza chembechembe nyekundu za damu na kusaidia ufanyaji kazi wa neva na mfumo wa kinga ya mwili.
Pia husaidia mwili kutengeneza kolajeni ambayo husaidia kufyoza madini chuma na hufanya kazi katika uzalishaji wa nishati mwilini.
Madini ya shaba hupatikaka kwa wingi kwenye ini, figo, moyo, ubongo na mfumo wa maskuloskeleto.
Mwili unahitaki kiwango sawia ili ufanye kazi vizuri, kuvurugika kwa kiwango cha madini haya huweza kuathiri ufanyaji kazi wa ubongo na ogani zingine.
Umuhimu wa kiafya wa madini ya shaba
Hupunguza kiwango cha kolestrol kwenye damu
Huongeza uzalishaji wa chembe nyeupe za dam una hivyo kusaidia mwili kupambana na maradhi
Huifanya mishipa kuwa imara na kufanya isivunjike kiurahisi
Hutengeneza kolajeni kwa wingi mwilini
Upungufu wa madini shaba
Upungufu wa madini ya shaba hutokea kwa nadra na huweza kusababishwa na mambo yafuatayo;
Matatizo ya ufyozwaji wa madini kwenye utumbo
Kutumia kwa wingi dawa nyongeza za vitamin C na zinki
Madhara ya upungufu wa madini shaba
Upungufu wa damu
Kuchuka kwa joto la mwili
Mifupa kuvunjika kiurahisi
Ngozi kukosa ulinzi
Matatizo katika tezi ya thairoidi
Uraisi wa kupata maambukizi
Vyanzo vya madini ya shaba
Mbegu za mazao mbalimbali
Maharagwe
Viazi
Amira
Mboga za kijani
Matunda yaliyokaushwa
Nyama za ini,figo na moyo
Pilipili manga
Vidonge vya madini shaba vipo na vinaweza kutumiwa kwa wagonjwa wenye upungufu wa madini haya. Ni vyema kutumia vyakula vyenye shaba kwa wingi kwanza ili kupunguza hatari ya kupungukiwa madini haya.
Ni asilimia ndogo sana ya watu huhitaji kutumia vidonge vya madini ya shaba.
Vidonge nyongeza vya madini ya shaba havipaswi tumika na dawa zifuatazo;
Baloxavir marboxil
Omadacycline
Penicillamine
Sarecycline
Aspirin
Ibuprofen
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:12:21
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
MedicalNewToday.Copper.https://www.medicalnewstoday.com/articles/288165 Imechukuliwa 13/4/2020
Medscape.Copper.https://emedicine.medscape.com/article/2087780-overview Imechukuliwa 13/4/2020
WebMd.Copper.https://www.webmd.com/vitamins-and-supplements/copper-your-health Imechukuliwa 13/4/2020
ReadersDigest.Copper.https://www.readersdigest.ca/health/healthy-living/health-benefits-copper/ Imechukuliwa 13/4/2020