top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Mangwella S, MD

Alhamisi, 16 Aprili 2020

Faida za madini ya Zinki mwilini
Faida za madini ya Zinki mwilini

Ni madini yanayofanya kazi nyingi mwilini, madini haya hayatengenezwi mwilini, ila yanapatikana kwenye vyakula. Unapaswa kula vyakula vyenye madini haya kwa wingi ili kuzuia upungufu wake na madhara yanayoweza kujitokeza.


Umuhimu wa zinki


Zinki huhitajika mwilini kwa ajili ya;


 • Shughuli za vimeng’enya

 • Kuimarisha mfumo wa kinga mwilini

 • Utengenezwaji wa protini

 • Utengenezwaji wa DNA

 • Kuponya vidonda

 • Ukuaji na maendeleo ya mwili

 • Kuzuia kuharisha kwa kuponya mfumo wa Gastrointestino


Madini haya hupatikana wa wingi kwenye mimea na vyakula vya Wanyama


Kazi za zinki mwilini


 • Husaidia kuchochea vimeng’enya zaidi ya 300 ambao hutumika katika umeng’enyaji wa chakula

 • Huimarisha mfumo wa kinga za mwili na kusaidia mwili upambane na maradhi.

 • Hutumika katika uzalishaji wa protini muhimu mwilini na utengenezwaji wa DNA

 • Huongeza kasi ya uponyaji wa vidonda

 • Hutumika kuondoa chunusi, watu wengi ambao hupata chunusi ni wale ambao wana madini ya zinc kwa uchache ,hivyo kutumia vyakula vyenye madini ya zinki au dawa mbadala huweza kutoa chunusi

 • Hupunguza inflamesheni kwenye seli


Dalili za upungufu wa zinki


 • Huathiri mfumo wa kinga ya mwili

 • Huathiri ukuaji na maendeleo ya mwili

 • Huchelewesha ukuaji kijinsia

 • Kutokwa na vipele kwenye ngozi

 • Kuhara

 • Vidonda kutokupona mapema


Vyanzo vya madini zinki


 • Samaki jamii ya shellfish

 • Nyama

 • Nyama za Wanyama jamii ya ndege

 • Mboga jamii ya kunde

 • Mayai

 • Mbegu zisizokobolewa

 • Baadhi ya mboga za majani kama bamiia,uyoga na kunde


Zipo dawa za mbadala za kutumia kwa mtu mwenye upungufu wa madini ya zinki


Dawa hizi hutolewa katika mfumo wa tembe, vidonge na maji


Dawa hizi zinapotolewa kwa wingi huweza kupelekea madhara kama;


 • Kichefuchefu

 • Kutapika

 • Kuharisha

 • Maumivu ya tumbo

 • Kubana kwa tumbo

 • Kupua kwa kinga ya mwili


Ili kuepuka dozi kubwa unapaswa kutumia kwa dozi jinsi ambavyo utakuwa umeelekezwa na daktari


Mama mjamzito na anayenyonyesha mahitaji ya madini haya huongezeka kufikia miligramu 11 hadi 12 kwa siku

Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:13:42
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. WebMd.Zinc.https://www.webmd.com/vitamins/ai/ingredientmono-982/zinc. Imechukuliwa 14/4/2020

 2. MedicalNewTodau.zinc.https://www.medicalnewstoday.com/articles/263176. Imechukuliwa 14/4/2020

 3. HealthLine.ZincMineral.https://www.healthline.com/nutrition/zinc. Imechukuliwa 14/4/2020

 4. Mayoclinic.Zinc.https://www.mayoclinic.org/drugs-supplements-zinc/art-20366112. Imechukuliwa 14/4/2020

bottom of page