top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, CO

Dkt. Sospeter M, MD

Jumamosi, 4 Desemba 2021

Jozi
Jozi

Jozi ni karanga zitokanazo na kokwa zinazopatikana kwenye matunda ya Jozi. Jozi imekua ikitumika kama chakula tangu enzi mpaka miaka hii imekua ikishauriwa kutumika kwa kuwa ni bora na salama kwa afya.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye jozi


  • Mafuta

  • Madini

  • Sukari

  • Nyuzilishe

  • Protini

  • Vitamini

  • Kabohaidreti

  • Maji


Viinilishe vinavyopatikana kwenye jozi yenye gramu 100


  • Nishati = 654kcal

  • Mafuta = 65g

  • Maji = 4.1g

  • Kabohaidreti = 14g

  • Sukari = 2.6g

  • Nyuzilishe = 6.7g

  • Protini = 15g


Vitamini zinazopatikana kwenye jozi yenye gramu 100


  • Vitamini A = 1mcg

  • Vitamini B1 = 0.34mg

  • Vitamini B2 = 0.2mg

  • Vitamini B3 = 1.13mg

  • Viatmini B5 = 0.6mg

  • Vitamini B9 = 98mcg

  • Vitamini C =1.3mg

  • Vitamini E =0.7mg

  • Vitamini K = 2.7mg


Madini yanayopatikana kwenye jozi yenye gramu 100


  • Kalisiamu = 98mg

  • Kopa = 1.6mg

  • Chuma = 2.9mg

  • Magnezium = 158mg

  • Manganese = 3.4mg

  • Fosfolasi = 346mg

  • Potassium = 441mg

  • Sodium = 2mg

  • Zinki = 3.1mg


Faida za jozi


Faida za kiafya za karanga ya jozi ni;


  • Kuimarisha afya ya uzazi kwa wanaume

  • Kimarisha na kuboresha afya moyo

  • Kupunguza uzito

  • Kuimarisha na kuboresha mishipa ya damu hivyo kukinga mwili dhidi ya shinikizo la juu la damu

  • Kuimarisha afya ya macho na kuongeza uwezo wa macho kwenye kuona

Imeboreshwa,
4 Desemba 2021, 15:37:13
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. Metabolism of Antioxidant and Chemopreventive Ellagitannins from Strawberries, Raspberries, Walnuts, and Oak-Aged Wine in Humans: Identification of Biomarkers and Individual Variability. Begoña Cerdá, Francisco A. Tomás-Barberán, and Juan Carlos Espín, J. Agric. Food Chem., 2005, 53 (2), pages 227–235,

  2. D. S. Vohra (1 June 2004). Bach Flower Remedies: A Comprehensive Study. B. Jain Publishers. p. 3. ISBN 978-81-7021-271-3.

  3. https://uc.xyz/14LzOm?pub=link [Beneficial effects of walnut consumption on human health: role of micronutrients - PubMed] Imepitiwa tarehe 30/11/2021

bottom of page