Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Benjamin L, MD
Jumatatu, 21 Machi 2022
Kiazi mviringo
Kiazi mviringo ni zao litokanalo na mizizi kutoka kwenye familia ya Solanaceae, zao hili huwa na faida nyingi kwa afya hiyo ni kutokana na uwepo wa virutubisho kwenye zao hili.
Ili kupata afya bora itakayotokana na utumiaji wa viazi mviringo, inashauriwa kisikaangwe bali kitumike kwa kuchemshwa/kupikwa tena kikiwa na maganda yake.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Kiazi Mviringo
Mafuta
Madini
Sukari
Nyuzilishe
Protini
Vitamini
Kabohaidreti
Maji
Kemikali muhimu kutoka kwenye Kiazi Mviringo
Kiazi mviringo kina kemikali muhimu Ziitwazo Butyrate na Phenolic Acid
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Kiazi mvingo chenye gramu 100
Nishati = 77kcal
Mafuta = 0.1g
Maji = 79.25g
Kabohaidreti = 17g
Sukari = 0.8g
Nyuzilishe = 2.1g
Protini = 2.1g
Vitamini zinazopatikana kwenye Kiazi Mviringo chenye gramu 100
Vitamini B1 = 0.81mg
Vitamini B2 = 0.32mg
Vitamini B3 = 1.061mg
Viatmini B5 = 0.295mg
Vitamini B6 = 0.298mg
Vitamini B9 = 15mcg
Vitamini C =19mg
Vitamini E =0.01mg
Vitamini K = 2mg
Madini yanayopatikana kwenye Kiazi Mviringo chenye gramu 100
Kalishiamu = 12mg
Kopa = 0.11mg
Madini Chuma = 0.81mg
Magineziamu = 23mg
Manganaizi = 0.153mg
Fosifolasi = 57mg
Potashiamu = 425mg
Sodiamu = 6mg
Zinki = 0.3mg
Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Viazi Mviringo
Huweka msawazo wa sukari mwilini.
Husaidia mfumo wa chakula na kulainisha choo.
Husaidia kuweka msawazo wa homoni mwilini.
Hupunguza uzito
Hupunguza kasi ya kupatwa na ugonjwa wa kansa
Imeboreshwa,
21 Machi 2022 16:25:23
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Potatoes. https://www.nutritionvalue.org/Potatoes%2C_raw%2C_flesh_and_skin_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 18 January 2022.
Camire ME, Kubow S, Donnelly DJ. Potatoes and human health. Crit Rev Food Sci Nutr. 2009 Nov;49(10):823-40. doi: 10.1080/10408390903041996. PMID: 19960391. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/19960391/. Imechukuliwa tarehe 18 January 2022.
Halton TL, Willett WC, Liu S, Manson JE, Stampfer MJ, Hu FB. Potato and French fry consumption and risk of type 2 diabetes in women. Am J Clin Nutr. 2006;83:284–90. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3650512/. Imechukuliwa tarehe 18 January 2022.