top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Lugonda S, MD

Alhamisi, 16 Desemba 2021

Kinywaji cha ngano na pichi
Kinywaji cha ngano na pichi

Kinywaji chenye asili ya Chile, huburudisha sana, kimetengenezwa kutokana na ngano iliyochemshwa na pichi zilizokaushwa juani ziitwazo huesillos. Hutoa hamirojo na protini ya ngano pamoja na vitamin na viuajisumu.


Maandalizi


  1. Loweka pichi zilizokaushwa juani kisha kuziacha kwa siku moja.

  2. Pika pichi zilizokaushwa juani kwa muda wa nusu saa katika maji yaliyoongezwa sukari (hasa isiyosafishwa au ya kahawia – piloncillo au panela, kwa kiasi kidogo) na kutia kijiti cha mdalasini au karafuu. Badala ya sukari, tumia shamu ya miwa au asali ya nyuki.

  3. Ongeza ngano iliyochemshwa na kunywa ikiwa baridi.

Imeboreshwa,
16 Desemba 2021 18:54:02
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

1. Sattar, et al. “Functional quality of optimized peach-based beverage developed by application of ultrasonic processing.” Food science & nutrition vol. 7,11 3692-3699. 14 Oct. 2019, doi:10.1002/fsn3.1227.


Shewry, et al. “The contribution of wheat to human diet and health.” Food and energy security vol. 4,3 (2015): 178-202. doi:10.1002/fes3.64.

bottom of page