top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, CO

Dkt. Benjamin L, MD

Jumatatu, 21 Machi 2022

Koliflawa
Koliflawa

Koliflawa ni mboga za majani kutoka kundi la Brassica oleracea, kwa mbali hutaka kufanana na Brocoli lakini tofauti yake ni kuwa huwa na kiini cheupe teketeke katikati ambacho ndo huliwa.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Koliflawa


  • Mafuta

  • Madini

  • Sukari

  • Nyuzilishe

  • Protini

  • Vitamini

  • Kabohaidreti

  • Maji


kemikali muhimu inayopatikana kwenye Koliflawa


Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Koliflawa ni sulforaphane na Ascobic Acid


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Koliflawa yenye gramu 100


  • Nishati = 23kcal

  • Mafuta = 0.1g

  • Maji = 93g

  • Kabohaidreti = 4.1g

  • Sukari = 2.1g

  • Nyuzilishe = 2.3g

  • Protini = 1.8g


Vitamini zinazopatikana kwenye Koliflawa yenye gramu 100


  • Vitamini A = 1mcg

  • Vitamini B1 = 0.42mg

  • Vitamini B2 = 0.052mg

  • Vitamini B3 = 0.410mg

  • Viatmini B5 = 0.508mg

  • Viatmini B6 = 0.173mg

  • Vitamini B9 = 44mcg

  • Vitamini C =44.3mg

  • Vitamini E =0.07mg

  • Vitamini K = 13.8mg


Madini yanayopatikana kwenye Koliflawa yenye gramu 100


  • Kalishiamu = 16mg

  • Kopa = 0.02mg

  • Madini Chuma = 0.32mg

  • Magineziamu = 9mg

  • Manganaizi = 0.132mg

  • Fosifolasi = 32mg

  • Potashiamu = 142mg

  • Sodiamu =15mg

  • Zinki = 0.17mg


Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Koliflawa


  • Huimarisha na kuzuia magonjwa yanayoathiri mfumo wa mmeng`enyo wa chakula

  • Huongeza kinga ya mwili na kulinda seli za mwili na kuongeza CD4

  • Husaidia kupunguza uzito na Kusaidia kuweka msawazo wa homoni mwilini

  • Hupunguza athari za kupatwa na kansa za aina mbalimbali.

  • Huzuia magonjwa mbalimbali yanayoathiri moyo

  • Husaidia ukuaji na utendaji kazi wa ubongo

  • Huongeza hamu ya kula na kuongeza hali ya damu kuganda pindi itokapo nje ya mishipa yad amu.

Imeboreshwa,
21 Machi 2022 19:45:47
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. Cauliflower. https://www.nutritionvalue.org/Cauliflower%2C_without_salt%2C_drained%2C_boiled%2C_cooked_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 17 January 2022.

  2. Miglio C, Chiavaro E, Visconti A, Fogliano V, Pellegrini N. Effects of different cooking methods on nutritional and physicochemical characteristics of selected vegetables. J Agric Food Chem. 2008 Jan 9;56(1):139-47. doi: 10.1021/jf072304b. Epub 2007 Dec 11. PMID: 18069785. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/18069785/. Imechukuliwa tarehe 17 January 2022.

  3. Jahangir M, Kim HK, Choi YH, Verpoorte R. Health-affecting compounds in Brassicaceae. Comprehensive Reviews in Food Science and Food Safety. 2009;8(2):31–43. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3793502/. Imechukuliwa tarehe 17 January 2022.

bottom of page