top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, CO

Dkt. Benjamin L, MD

Jumatatu, 21 Machi 2022

Letusi
Letusi

Letusi ni mmea wa msimu unaotoka kwenye familia ya Astderaceae kundi la Lactuca. Letusi imekua ikitumika kama mboga mboga lakini pia kama kiungo kwenye kachumbari hiyo kutokana na harufu yake pia virutubisho vilivyopo ndani yake.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Letusi


  • Mafuta

  • Madini

  • Sukari

  • Nyuzilishe

  • Protini

  • Vitamini

  • Kabohaidreti

  • Maji


Kemikali muhimu zinazopatikana kwenye Letusi


Kemikali muhimu zinazopatikana kwenye Letusi ni Terpenes na Cardenolides.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Letusi zenye gramu 100


  • Nishati = 14kcal

  • Mafuta = 0.1g

  • Maji = 95.5g

  • Kabohaidreti = 3g

  • Sukari = 2g

  • Nyuzilishe = 1.2g

  • Protini = 0.9g


Vitamini zinazopatikana kwenye Letusi zenye gramu 100


  • Vitamini A = 25mcg

  • Vitamini B1 = 0.041mg

  • Vitamini B2 = 0.25mg

  • Vitamini B3 = 1.123mg

  • Viatmini B5 = 0.091mg

  • Vitamini B6 = 0.042mg

  • Vitamini B9 = 29mcg

  • Vitamini C = 2.8mg

  • Vitamini E =0.18mg

  • Vitamini K = 24.1mg


Madini yanayopatikana kwenye Letusi zenye gramu 100


  • Kalishiamu = 18mg

  • Kopa = 0.03mg

  • Madini Chuma = 0.41mg

  • Magineziamu = 7mg

  • Manganaizi = 0.125mg

  • Fosifolasi = 20mg

  • Potashiamu = 141mg

  • Sodiamu = 10mg

  • Zinki = 0.15mg


Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Letusi


  • Husaidia kuimarisha kinga ya mwili

  • Husaidia kukupa usingizi mwororo

  • Huimarisha seli hai nyeupe za damu

  • Husaidia kuzuia ugonjwa wa moyo na shinikizo la juu la damu

  • Huzuia/kutibu baadhi ya magonjwa ya Ngozi yatokanayo na fangasi

  • Husaidia kuondoa tatizo la sonona

Imeboreshwa,
21 Machi 2022 19:53:16
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. Lettuce. https://www.nutritionvalue.org/Lettuce%2C_raw%2C_cos_or_romaine_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.

  2. Yang X, Gil MI, Yang Q, Tomás-Barberán FA. Bioactive compounds in lettuce: Highlighting the benefits to human health and impacts of preharvest and postharvest practices. Compr Rev Food Sci Food Saf. 2022 Jan;21(1):4-45. doi: 10.1111/1541-4337.12877. Epub 2021 Dec 21. PMID: 34935264. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/34935264/. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.

  3. Lettuce romaine calm and manage our glycemia: adding leafy greens to a meal may improve postprandial metabolism. Written by Gregory C. Henderson. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7029024/. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.

bottom of page