top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Mangwella S, MD

Jumapili, 22 Novemba 2020

Madini muhimu mwilini
Madini muhimu mwilini

Madini ni moja ya virutubisho muhimu kwenye mwili wa binadamu, husaidia chembe hai ziweze kufanya kazi zake ipasavyo. Kwa kawaida mwili wa binadamu huwa hauzalishi madini, hivyo unahitaji kupata madini kupitia chakula cha mimea pamoja na kunywa maji. Madini hufanya kazi nyingi sana ndani ya mwili wa binadamu licha ya kuwa huhitajika kwa kiasi kidogo tu. Makala hii imezungumzia kuhusu madini yanayopatikana ndani ya mwili wa binadamu


Ni madini gani yapo ndani ya mwili wa binadamu?


Madini yaliyo ndani ya mwili wa binadamu yamegawanyika katika makundi mawili, madini yanayohitajika kwa kiasi kikubwa nay ale yanayohitajika kwa kiasi kidogo. Madini yanayohitajika kwa kiasi kikubwa huwa mengi kwenye damu kuliko yale yanayohitajika kwa kiasi kidogo


Madini yanayohitajika kwa kiasi kikubwa


Kalisiamu


Kalisiamu hupatikana kwa wingi kwenye mazao ya maziwa, maziwa, mayai, samaki wa kusindikwa kama sardine na salmon wenye mifupa, mboza za kijani, karanga, mbegu za mimea, tofu na sinamoni


Fosforasi


Madini haya hupatikana kwenye yakula vya nyama nyekundu, vyakula vyenye maziwa, samaki, kuku na ndege wengine, mkate, mchele na shairi


Potasiamu(magadi)


Madini haya hupatikana kwenye vyakula kama viazi vitamu, nyanya, maharagwe, mimea jamii ya kunde, viazi mviringo, vyakula vyenye maziwa, vyakula vya baharini, ndizi, karoti na machungwa.


Sodiam (madini chumvi)


Hupatikana kwa wingi kwenye chumvi ya chakula9hupatikana kama sodiam kloraidi), mboga za majani za baharini, maziwa na spinachi


Magnesi


Magnesi hupatikana kwenye vyakula kama Spinachi, mimea jamii ya kunde, karanga, mbegu za mimea, mbegu zisizokobolewa, karanga za kusaga na parachichiMadini yanayohitajika kwa kiasi kidogo


Chuma


Hupatikana kwenye nyama, vyakula vya baharini, karanga mbalimbli, maharagwe, na chokoleti nyeusi


Chlorine


Hupatikana kweney chumvi ya chakula kama muunganiko wa sodiamu kloraidi


Kobalti


Hupatikana kwa kula wanyama na mazao ya wanyama kama mayai n.k


Shaba


Hupatikana kwenye vyakula kama maini, vyakula vya baharini, karanga, mbegu zisizokobolewa, kunde


Zinki


Hupatikana kwenye nyama nyekundu, nyama jamii ya ndege, karanga, mbegu zisizokobolewa na vyakula vya maziwa


Manganizi


Hupatikana kwenye kunde, karanga, vyakula vya mbegu zisizokobolew, mboga za majani, majani ya chai na kahawa.


Molybdenum


Hupatikana kwenye mbegu zisizokobolewa, kunde na karanga


Madini joto


Hupatikana kwenye magugu maji ya baharini, mayai na chumvi ilotiwa madini joto


Seleniamu


Hupatikana kwenye vyakula vya habarini, nyama za viungo vya ndani vya wanyama kama maini n.k, nyama, mayai, na maziwa ya ng’ombe.

Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:08:25
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

bottom of page