top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

Dkt. Peter A, MD

Ijumaa, 17 Desemba 2021

Maji
Maji

Mwili unahitaji kiwango sahihi cha maji ili kuendesha shughuli mbalimbali zinazokufanya uwe na afya njema. Mahitaji ya maji hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Makala hii inaweza kukusaidia kunywa maji ya kutosha mahitaji ya mwili wako.


Ni kiasi gani cha maji unachotakiwa kunywa kila siku?.


Ni swali jepesi lakini halina majibu rahisi. Tafiti zimependekeza viwango tofauti tofauti miaka mingi, lakini kiukweli, mahitaji yako ya maji hutegemea vitu vingi, ikiwemo afya yako, kazi unazofanya na mahari gani unaishi.

Ingawa hakuna kanuni moja inayomhusu kila mtu, kujua kuhusu mahitaji ya mwili wako yatakusaidia kukadilia ni kiasi gani unachohitaji kunywa kwa kila siku

Faida za kiafya za maji

​​

Maji ni kemikali kubwa na ya msingi katika mfumo wako wa chembe hai, asilimia 60 ya uzito wa binadamu umechangiwa na maji. Kila mfumo ndani ya mwili hutegemea maji ili kufanya kazi. Mfano, maji husafisha sumu kutoka nje ya viungo muhimu vya mwili, hubeba virutubisho kuingiza ndani ya chembe hai, na huzalisha mazingira ya unyevu kwenye pua, sikio na koo pia.

Upungufu wa maji hupelekea kukaukiwa kwa mwili, hali hii hutokea endapo huna kiwango cha kutosha kufanya kazi za kawaida katika mwili. Upungufu wa maji hata kwa kiwango kidogo husababisha kufanya mwili ujisikie mchovu.

Kiasi gani cha maji unahitaji?

Kila siku unapoteza maji kupitia pumzi, hewa unayotoa, kupitia mkojo na kinyesi. Ili mwili wako ufanye kazi kisawa sawa unahitaji kufidia kiwango hicho kinachotoka kwa kunywa vinywaji na vyakula vyenye maji.

Kwa hivyo ni kiasi gani cha maji unachotakiwa kutumia, kwa mtu mwenye afya njema na anaishi kwenye ukanda wa joto? Institute of medicine imeelezea kwa mwanaume ni kiasi cha vikombe 13 ambavyo ni sawana lita 3 kwa masaa 24 na kwa wanawake ni vikombe 9 ambavyo ni sawa na lita 2.2 kwa masaa 24

Vipi kuhusu ushauri wa kunywa glasi 8 kwa siku?

Kila mmoja amesikia ushauri, kunywa glasi nane kwa siku, hii ukikadilia ni sawa na lita 1.9, ambayo si tofauti sana na kiwango kilichoshauriwa na institute of medicine, ingawa kanuni hii ya glasi 8 haijatetewa na ushahidi mkubwa, imebaki kuwa maarufu kwa sababu ni rahisi kuikumbuka. Kumbuka kwamba kiasi kinatakiwa kurekebishwa na kuwa . kunywa ounce 8 kwa siku kwa sababu majimaji yote huhesabika kwenye kiwango cha jumla cha siku


Mambo yanayoongeza mahitaji ya maji mwilini


Unaweza kuhitajika kurekebisha kiwango cha maji unayotakiwa kunywa ikitegemea shughuli gani unayofanya,hali ya hewa ya sehemu unayoishi, hali yako ya afya na kama una ujauzito ama unanyonyesha


Mazoezi

Kama unafanya mazoezi yanayokufanya utoe jasho unatakiwa kunywa kiwango cha ziada cha maji karibia kikombe 1 na nusu hadi 2 na nusu yaani (mililita 400 hadi 600) .lakini mazoezi magumu zaidi yanayotumia zaidi ya lisaa kama kukimbia riadha huhitaji kiwango kikubwa zaidi


Mazoezi magumu

Kwenye kipindi cha mazoezi makali, ni vema kutumia maji ya mazoezi ambayo huwa na madini ya sodium, ambayo husaidia kufidia kiwango cha madini hayo kinachopotea kupitia jasho na kukufanya usipungukiwe na madini hayo mwilini. Ukipungukiwa na madini hayo unaweza kupata shida sana mwilini


Mazingira/hali ya hewa

Ikiwa unaishi kwenye hali ya hewa ya joto huweza kukufanya utoe jasho sana na utahitaji kiasi kikubwa zaidi cha maji. Kuishi ndani ya nyumba yenye hita hufanya hewa iwe ya moto na hivyo unapoteza kiwango cha maji mwilini hivyo utahitaji kiwango zaidi ili kufidia kiwango cha kawaida. Hata hivyo kuishi mita zaidi ya 25000 kutoka usawa wa bahari huweza amsha kukojoa sana na kupumua kwa haraka na hivyo kusababisha kupoteza akiba ya mwili


Hali yako ya kiafya

Ukiwa na homa, kutapika ama kuhara, mwili wako unapoteza kiwango zaidi cha maji, katika hali hii unahitajika kunywa maji zaidi. Wakati mwingine dakitari wako atakupatia ORS.kuna baadhi ya matatizo/magonjwa ya moyo kama vile moyo kufeli kufanya kazi, mtu anatakiwa asinywe kiwongo kikubwa cha maji hivyo kama una tatizo kama hili wasiliana na daktari wako


Mjamzito na mama anayenyonyesha.

Wanawake wanaonyonyesha ama walio wajawazito wanahitaji kunywankiwango cha maji cha kutosha ili kufanya mwili ufanye kazi ipasavyo. Hii ni kwa sababu kiwango kikubwa cha maji hutumika mtoto anapokuwa ananyonya ama.institute of medicine wamependekeza wanawake wajawazito wanywe lita 2.3 ya maji kila siku na wanawake wanaonyonyesha wanywe lita 3.1ya maji kila siku


Vyanzo vya maji ya kunywa


Maji ya bomba

Huhitaji kutegemea maji ya bomba tu ama ya kununua kama chanzo chako cha maji ya kunywa, kwani kile unachokula pia kama kina maji huchangia kuupa mwili wako maji. Mfano kula matunda yenye majimaji kama tango, nanai, tikiti maji chungwa n.k huchangia ongezeko la maji kwenye mwili. Kwa kifupi chakula na vitu vya majimaji huchangia asilimia ishiriri ya maji unayotakiwa kupata.


Vinywaji

Vinywaji kama maziwa, juisi na soda pia huwa na maji mengi, na hata vile bia kahawa na chai huchangia pia kwa kiasi kiasi katika kuupa mwili maji


Kunywa maji, usipungukiwe maji


Kikawaida , kama ukinywa maji ya kutosha kiasi kwamba usisikie kiu na mkojo wako ukawa safi au kuwa njano kiasi na umekunywa lita moja na nusu kwa siku basi upo katika mstari myoofu, na kiwango cha maji kipo katika kiasi sahihi. Ikiwa unashaka basi onana na daktari ili akushauri kiwango cha maji kinachotosha kwa mwili wako.

Imeboreshwa,
17 Desemba 2021 09:56:08
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. Barry M. Popkin et al.. Water, Hydration and Health. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2908954/. Imechukuliwa 15.02.2021

  2. Carmen B. Franse et al. Factors associated with water consumption among children: a systematic review. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6693220/. Imechukuliwa 15.02.2021

  3. Unaiza Faizan et al. Nutrition and Hydration Requirements In Children and Adults. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK562207/. Imechukuliwa 15.02.2021

  4. Lawrence E. Armstrong et al. Water Intake, Water Balance, and the Elusive Daily Water Requirement. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6315424/. Imechukuliwa 15.02.2021

  5. Dr. Julia MW Wong et al. Effects of advice to drink 8 cups of water per day in adolescents with overweight or obesity: a randomized trial. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5530362/. Imechukuliwa 15.02.2021

  6. Arend-Jan Meinders et al. How much water do we really need to drink?. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/20356431/#. Imechukuliwa 15.02.2021

bottom of page