top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, MD

Dkt. Benjamin L, MD

Ijumaa, 17 Desemba 2021

Maziwa ya lozi
Maziwa ya lozi

Maziwa ya lozi bado ni mbadala mwingine wa maziwa ya ng’ombe, hasa pale yale ya awali yanapoleta mzio au kutovumilika. Hata hivyo, licha ya kuwa na faida kuliko maziwa ya ng’ombe, huwa na virutubishi kwa kiasi kidogo. Baadhi ya bidhaa za kibiashara za maziwa ya lozi zimeongezwa kalisi na vitamin A, D na B12. Dosari ya maziwa ya kibiashara ni kwamba huwa na sukari nyingi ya kuongezea.


Sifa


 • Kando ya zile zote zinazohusisha maziwa ya mimea [uk.28],maziwa ya lozi:

 • Yana utajiri wa vitamini B na vitamini E.

 • Chanzo cha kalisi ,magnesi,na potasiamu.

 • Uwezo wa kumeng’enya chakula.

 • Yanafaa kurudishia madini baada ya kupotea kutokana na maradhi ya tumbo au kuharisha .

 • Yanapendekezwa kutumika kwenye matukio ya mibabuko[ukurutu]utotoni.

 • Kiasi kidogo cha lehemu.

 • Inasaidia kustawisha bakteria rafiki kwenye utumbo


Viungo


Kwa milo mine yenye mililita 250 kwa kila mmoja unapaswa kuwa na viungo vifuatavyo;


 • Lozi gram 250

 • Tende 4-6 au kiganja cha zabibu kavu zisizo na mbegu au vijiko viwili vya chakula vya molasi au sukari guru.

 • Vikombe vinne vya maji.

 • Nusu kijiko cha chai cha mdalasini au vanilla


Maandalizi


 • Taratibu za maandalizi hufanana na uandaaji wa maziwa ya mimea mingine kwa ujumla. Lozi zinaweza kumenywa kabla ya kusagwa baada ya kuzibabua kwenye maji yanayochemka.

 • Changanya viungo vyote pamoja kasha weka kwenye kisagio cha sharubati na kusaga mpaka itakapokuwa laini.


Onyo

Ingawa kwa kiwango kidogo kuliko maziwa ya ng’ombe ,soya ,hazeli au lozi yanaweza kuleta mzio kwa watu wepesi kupatwa .


Maziwa ya lozi kwa watoto


Maziwa ya lozi yanapendekezwa sana kwa watoto katika tukio la kuharisha au mibabuko ya ngozi.


Kila mlo (bilauri au kikombe cha milimita 250) kina;


 • Niahati --Kalori 91kg, 5%

 • Sukari --15 kg, 17%

 • Mafuta --2.5kg, 4%

 • Mafuta kinaifu-- 0g, 0%

 • Sodium-- 0.15kg, 6%

 • Protini-- 1kg, 2%

 • Nyuzilishe -- 1g, 4%

Imeboreshwa,
17 Desemba 2021 09:49:55
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Vanga,et al. “How well do plant based alternatives fare nutritionally compared to cow's milk?.” Journal of food science and technology vol. 55,1 (2018): 10-20. doi:10.1007/s13197-017-2915-y

 2. Cuppari C,et al. ALMOND MILK: A POTENTIAL THERAPEUTIC WEAPON AGAINST COW’S MILK PROTEIN ALLERGY. J Biol Regul Homeost Agents. 2015 Apr-Jun;29(2 Suppl 1):8-12. PMID: 26634581.

bottom of page