Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Lameck P, HM
Dkt. Sospeter M, MD
Jumapili, 19 Desemba 2021
Maziwa ya shayiri
Ingawa haina protini nyingi na kalisi kama ya soya, humeng’enywa vizuri zaidi na pia huvumiliwa na tumbo lenye matatizo.
Ingawa yanapatikana katika maduka mengi,yakiwa yameandaliwa tayari ,maziwa ya shayiri au vinywaji vya shayiri zinaweza kutengenezwa kwa urahisi nyumbani.Hatakama inaleta gramu 1.2 tu za protini katika kila gramu 100 [maziwa ya soya na ng’ombe kariba gramu 3 kwa gramu mia],maziwa ya shayiri pia yanageuka kuwa na virutubishi na mmeng’enyo mzuri.
Sifa
Kando ya zile za kawaida kwa maziwa ya mimea yote, maziwa ya shayiri;
Ni chanzo cha protini na vitamin B
Ni rahisi kumeng’enywa kuliko maziwa ya soya na ng’ombe .
Ni kitulizo cha tumbo na utumbo.
Kwa ujumla huvumiliwa na wale wagonjwa wenye matumbo yasiyovumilia gluteni.
Hayana mizio na yanafaa kwa wale wenye mzio kwa maziwa ya ng’ombe.
Yana nyuzinyuzi nyingi aina ya glykani zinazoyeyuka, zikiwa na uwezo wa kustawisha na kuwezesha uwiano wa ukuaji wa bakteria rafiki kwenye utumbo.
Hupunguza kiwango cha lehemu na mafuta ya triglyceride.
Huongeza umakini na kazi ya akili
Viungo
Ili kuandaa milo minne yenye wastani wa mililita 250 kila mlo unapaswa kuwa na;
Gramu 150 za chenga za shayiri isiyokoborewa
Tende 6 au tumia zabibu kavu isiyo na mbegu kiganja kimoja au molasi vijiko viwili vya chakula au sukari guru
Vikombe 4 vya maji
Mdalasini nusu kijiko cha chai cha
Maandalizi
Weka kwa pamoja tende, zabibu kavu au sukari katika kikombe kimoja cha maji kisha tia kwenye mashine ya kusagia matunda na usage mpaka upate mchanganyiko laini.
Imeboreshwa,
19 Desemba 2021 10:23:24
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Fulgoni, Victor L 3rd et al. “Oatmeal-Containing Breakfast is Associated with Better Diet Quality and Higher Intake of Key Food Groups and Nutrients Compared to Other Breakfasts in Children.” Nutrients vol. 11,5 964. 27 Apr. 2019, doi:10.3390/nu11050964.
Onning G, et al. Effects of consumption of oat milk, soya milk, or cow's milk on plasma lipids and antioxidative capacity in healthy subjects. Ann Nutr Metab. 1998;42(4):211-20. doi: 10.1159/000012736. PMID: 9745107.