top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. PEter R, Co

Jumapili, 27 Machi 2022

Shamari
Shamari

Ni zao litokanalo na miti ya maua yenye rangi ya njano na majani yenye manyoya manyonya yenye mfanano na zao la Karoti kutoka familia ya Apiaceae. Ni maarufu kutokana na harufu yake nzuri pindi itumikapo kwenye chakula baada ya kupikwa.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Shamari


 • Mafuta

 • Madini

 • Sukari

 • Nyuzilishe

 • Protini

 • Vitamini

 • Kabohaidreti

 • Maji


Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Shamari


Shamari ina kemikali muhimu ambazo ni Rosmarinic Acid na Quercetin na Apigenin.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Shamari yenye gramu 100


 • Nishati = 31kcal

 • Mafuta = 0.2g

 • Maji = 90.21g

 • Kabohaidreti = 7.3g

 • Sukari = 3.9g

 • Nyuzilishe = 3.1g

 • Protini = 1.2g


Vitamini zinazopatikana kwenye Shamari yenye gramu 100


 • Vitamini A = 48mcg

 • Vitamini B1 = 0.01mg

 • Vitamini B2 = 0.032mg

 • Vitamini B3 = 1.640mg

 • Viatmini B5 = 0.232mg

 • Vitamini B6 = 0.47mg

 • Vitamini B9 = 27mcg

 • Vitamini C =12mg

 • Vitamini E =0.58mg

 • Vitamini K = 62.8mg


Madini yanayopatikana kwenye Shamari yenye gramu 100


 • Kalishiamu = 49mg

 • Kopa = 0.07mg

 • Madini Chuma = 0.73mg

 • Magineziamu = 17mg

 • Manganaizi = 0.191mg

 • Fosifolasi = 50mg

 • Potashiamu = 414mg

 • Sodiamu = 52mg

 • Zinki = 0.2mg


Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Shamari


 • Kupunguza homa, Kuzuia homa ya ini na kuzuia athari ya kupatwa na ugonjwa wa kansa aina mbalimbali

 • Kupunguza hamu ya kula mara kwa mara hivyo kupelekea kusaidia kwenye Kupunguza uzito.

 • Kuimarisha kinga ya mwili na Kuzuia baadhi ya magonjwa yasabishwayo na virusi Pamoja na bakteria

 • Kupunguza athari yakupatwa na magonjwa ya mda mrefu kama kansa, kisukari na shinikizo la juu la damu.

 • Kuimarisha afya ya moyo

 • Kusaidia wamama wanaonyinyesha kwa kuongeza kiwango cha uzalishwaji wa maziwa

 • Kuimarisha mfumo wa fahamu na kusaidia kutunza kumbukumbu

 • Kusaidia kupunguza athari wapatazo wamama waliofikia ukomo wa kuona siku zao

Imeboreshwa,
27 Machi 2022 16:09:51
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Fennel . https://www.nutritionvalue.org/Fennel%2C_raw%2C_bulb_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 12 January 2022.

 2. Ghorbani A. Studies on pharmaceutical ethnobotany in the region of Turkmen Sahra, north of Iran (Part 1): general results. J Ethnopharmacol. 2005 Oct 31;102(1):58-68. doi: 10.1016/j.jep.2005.05.035. PMID: 16024194. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/16024194/. Imechukuliwa tarehe 12 January 2022.

 3. . Oktay M, Gülçin I, Küfrevioglu ÖI. Determination of in vitro antioxidant activity of fennel (Foeniculum vulgare) seed extracts. LWT-Food Science and Technology. 2003;36(2):263–271. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4137549/#!po=0.220264. Imechukuliwa tarehe 12 January 2022.

bottom of page