top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Peter A, MD

Ijumaa, 22 Oktoba 2021

Tofaa
Tofaa

Faida za tunda tofaa


Moyo na mishipa ya damu

Huwa na kemikali ambazo Huweza zuia kutolewa kwa mafuta kutoka kwenye hifadhi yake na hivo huzuia mafuta kukusanyika katika damu ambayo ni kihatarishi cha magonjwa ya moyo.Mafuta yanapojirundika katika mishipa ya damu husababisha mgando katika mishipa na kuziba ama mishipa ya damu kuwa na njia ndogo,hali hii hupekekea kupanda kwa shinikizo la damu na magonjwa mengine mengi ya moyo na mishipa ya damu

Tofaa pia huwa na vitamin C na hivyo huleta faida za vitamin hiyo

Kudhibiti sukari katika damu

Katika mifumo tofauti , kemikali ya polyphenol iliyo ndani ya tufaha huweza kurekebisha umengenyaji wa chakula katika mfumo wa chakula na ndani ya chembe hai za mwili.

Kemikali ya Quercetin na zingine flavonoids hupunguza umengenyaji wa wanga na ufyonzwaji wa sukari baada ya kumengenywa

Huongeza utendaji kazi wa kongosho na hivo huzalisha kwa wingi homoni ya insulin inayopelekea kutumika na kupungua kwa sukari katika damu na kusababisha kuweka kiwango cha sukari kwenye hari nzuri

Husaidia kuongezeka kwa hisia ya chembe chembe zinazofyonza sukari na hivyo sukari hufayonzwa kutoka kwenye damu na kuingia kwenye chembechembe hizo na kudhibit sukari mwilini

Mbegu za tofaa huwa na vitamin B17 ambayo huweza kutumika kama dawa ya saratani ikitumiwa kwa usahihi.


Hitimisho


Makala hizi huboreshwa mara kwa mara, tembelea siku nyingine kusoma maelezo yaliyoongezeka.

Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 10:55:31
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

Boyer, et al. “Apple phytochemicals and their health benefits.” Nutrition journal vol. 3 5. 12 May. 2004, doi:10.1186/1475-2891-3-5
bottom of page