Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Mangwella S, MD
Jumamosi, 4 Desemba 2021
Ubuyu
Wataalamu wa afya wanautizama ubuyu kama tiba na chakula cha chembe hai za binadamu kwani umekua na faida nyingi sana kutokana na uwepo wa virutubisho muhimu kwa afya. Tunda hili hufahamika kuwa moja ya tunda lenye kiwango kikubwa cha viuasumu, matumizi yake ya mara kwa mara hukinga magonjwa sugu kama magonjwa ya moyo, mishipa ya damu na saratani.
Unaweza kupata wapi ubuyu?
Ubuyu pia unapatikana sehemu mbalimbali kama kwenye masoko, supamaketi, mpaka mitaani.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye ubuyu
Mafuta
Madini
Vitamini
Protini
Nyuzilishe
Kabohaidreti
Maji
Viinilishe katika gramu 100 za ubuyu
Gramu 100 za ubuyu huwa na;
Nishati = 250kcal
Kabohaidreti = 80g
Protini = 3.7g
Nyuzilishe = 45g
Maji = 11g
Mafuta = 0.5g
Sukari = 4.7g
Madini katika gramu 100 za ubuyu
Gramu 100 za ubuyu huwa na;
Kalishiamu = 342mg
Madini Chuma = 8.4mg
Magineziamu = 158mg
Phosifolasi = 47mg
Potashiamu = 2189mg
Sodiamu = 10mg
Zinki = 1mg
Vitamini katika gramu 100 za ubuyu
Gramu 100 za ubuyu huwa na;
Vitamini B1 = 0.03mg
Vitamini B2 =0.074mg
Vitamini B3 = 20mg
Vitamini B6 = 2.4mg
Vitamini C = 173mg
Kemikali muhimu kwenye ubuyu
Ubuyu huwa na kiasi kikubwa cha antioxidants na polyphenol zinazosaidia kuzuia na kudhibiti magonjwa ya moyo, shambulio binafsi la mfumo wa kinga, kisukari na saratani.
Faida za ubuyu
Kula ubuyu husaidia;
Kuongeza hamu ya kula
Kupunguza uzito
Kusawazisha kiwango cha sukari mwilini
Kuimarisha na kuboresha mfumo wa mmeng`enyo wa chakula
Imeboreshwa,
4 Desemba 2021, 17:26:34
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Osman, M. A. (2004). "Chemical and nutrient analysis of baobab (Adansonia digitata) fruit and seed protein solubility". Plant Foods Hum Nutr. 59 (1): 29–33.
Gardner, et al. May (2011). Heritage Trees of Penang. Penang: Areca Books. ISBN 978-9-675-71906-6.
Adrian Patrut et al. (2018) The demise of the largest and oldest African baobabs. Nature Plants 4: 423–426.
Rahul J, et al. Adansonia digitata L. (Baobab): A review of traditional information and taxonomic description. Asian Pac. J. Trop. Biomed. 2015;5:79–84.
Ghoneim M.A, et al. Protective effect of Adansonia digitata against isoproterenol-induced myocardial injury in rats. Anim. Biotechnol. 2016;27:84–95.
Vertuani S, et al. Antioxidant capacity of Adansonia digitata fruit pulp and leaves. Acta Phytother. 2002;V:2–7.
Braca, Alessandra et al. “Phytochemical Profile, Antioxidant and Antidiabetic Activities of Adansonia digitata L. (Baobab) from Mali, as a Source of Health-Promoting Compounds.” Molecules (Basel, Switzerland) vol. 23,12 3104. 27 Nov. 2018, doi:10.3390/molecules23123104