Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Jumapili, 27 Machi 2022
Ufuta
Ufuta ni mbegu zitokanazo na mmea wa ufuta mmea wa maua unaopatikana kwenye kundi Sesamum. Mbegu za hizi zinafaida lukuki kwa afya ya mlaji hyo ni kutokana na virutubisho ilivyonavyo.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Ufuta
Mafuta
Madini
Sukari
Nyuzilishe
Protini
Vitamini
Kabohaidreti
Maji
Kemikali muhimu zinazopatikana kwenye Ufuta
Kemikali muhimu zinazopatikana kwenye ufuta ni Pinoresinol,Lignans, Cysteine na Methionine.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Ufuta wenye gramu 100
Nishati = 565kcal
Mafuta = 48g
Maji = 3.3g
Kabohaidreti = 26g
Nyuzilishe = 14g
Protini = 17g
Vitamini zinazopatikana kwenye Ufuta Wenye gramu 100
Vitamini B1 = 0.803mg
Vitamini B2 = 0.251mg
Vitamini B3 = 4.581mg
Viatmini B5 = 0.051mg
Vitamini B6 = 0.802mg
Vitamini B9 = 98mcg
Madini yanayopatikana kwenye Ufuta wenye gramu 100
Kalishiamu = 989mg
Kopa = 2.47mg
Madini Chuma = 14.76mg
Magineziamu = 356mg
Manganaizi = 2.496mg
Fosifolasi = 638mg
Potashiamu = 475mg
Sodiamu = 11mg
Zinki = 7.16mg
Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Ufuta
Kusaidia kupunguza tatizo la uzito uliopitiliza
Kusaidia punguza rehemu kwenye damu hivyo kupunguza athari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo.
Kujenga mwili hiyo kutokana na uwepo wa protini kwa wingi.
Kuweka msawazo wa shinikizo la damu mwilini
Kuimarisha mifupa, Kusaidia kuongeza hamu ya kula Pamoja na Kusaidia kuongeza kinga ya mwili.
Kusaidia kuweka msawazo wa kiwango cha sukari kwenye damu
Kusaidia kupunguza athari zitokanazo na baridi yabisi ikiwamo maumivu.
Imeboreshwa,
27 Machi 2022 17:35:32
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Sesame_seeds. https://www.nutritionvalue.org/Seeds%2C_dried%2C_whole%2C_sesame_seeds_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 1 February 2022.
Gouveia Lde A, Cardoso CA, de Oliveira GM, Rosa G, Moreira AS. Effects of the Intake of Sesame Seeds (Sesamum indicum L.) and Derivatives on Oxidative Stress: A Systematic Review. J Med Food. 2016 Apr;19(4):337-45. doi: 10.1089/jmf.2015.0075. PMID: 27074618. Imechukuliwa tarehe 1 February 2022. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/27074618/. Imechukuliwa tarehe 1 February 2022.
Khadem Haghighian M, Alipoor B, Malek Mahdavi A, Eftekhar Sadat B, Asghari Jafarabadi M, Moghaddam A. Effects of sesame seed supplementation on inflammatory factors and oxidative stress biomarkers in patients with knee osteoarthritis. Acta Med Iran. 2015;53(4):207-13. PMID: 25871017. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/25871017/. Imechukuliwa tarehe 1 February 2022.
Hong L., Yi W., Liangliang C., Juncheng H., Qin W., Xiaoxiang Z. Hypoglycaemic and hypolipidaemic activities of sesamin from sesame meal and its ability to ameliorate insulin resistance in KK-Ay mice. J. Sci. Food Agric. 2012;93. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7584802/. Imechukuliwa tarehe 1 February 2022.