top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Peter A, MD

Jumatano, 10 Novemba 2021

Vitamin
Vitamin
Vitamin ni nini?

​

Vitamin ni kampaundi za kikaboni zinazohitajika kwa kiasi kidogo mwilini ili kufanikisha shughuli mbalimbali za kifiziolojia mwilini.

​

Mwili uhitaji kupata vitamin kutoka kwenye chakula, na miili ya binadamu huna uwezo kuzalisha vitamin kwa haraka ili kukidhi mahitaji yake ya kila siku.


Sifa za vitamin

​

Vitamin huwa na sifa kuu tatu ambazo ni;

​

  • Huwa ni kiungo asilia kwenye vyakula na hupatikana kwa kiwango kidogo sana

  • Uhutajika katika kuendesha kazi za kifiziolojia mwilini kama(ukuaji wa mwili, uzazi, uponyaji wa mwili, kupambana na maradhi n.k)

  • Zikikosekana mwilini udhaifu unaotokana na ukosefu wa vitamin husika hutokea.

​

Vitamin zimegawanyika kwenye makundi mawili makuu, vitamin zinazoweza kuchanganyika na maji, na zile ambazo hazichanganyiki na maji

​

Vitamin hufanya kazi kubwa mwilini ikiwa pamoja na kuwezesha vimengenya vya mwili kufanya kazi zake.


Kwanini unatakiwa kula vitamin kwa kiwango kinachotosha?

​

Majibu ni kwamba upungufu wa vitamin husababisha au kuleta magonjwa sugu mwilini

Aina za vitamin


Kuna aina mbili za vitamin, vitamin zinazochanganyika na zile zisizochanganyika na maji.


Vitamin zinazochanganyika na maji

Idadi ya vitamin zinazoweza kuchanganyika na maji hufikia 9 zikiwa pamoja na


  • Vitamin B1

  • Vitamin B2

  • Vitamin B3

  • Vitamin B5

  • Vitamin B6

  • Vitamin B9

  • Vitamin B12

  • Vitamin C


Vitamini zisizochanganyika na maji

​

Vitamin ambazo hazichanganyiki na maji (huchanganyika na mafuta) ni;


  • Vitamin A

  • Vitamin D

  • Vitamin E

  • Vitamin K

​

Katika makala haya utaelezewa umuhimu wa vitamin, zinapatikana wapi nini madhara ya upungufu na madhara ya kula dozi kubwa kupita kiasi ya vitamini hizi.

Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 10:59:27
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. NHS. https://www.nhs.uk/conditions/vitamins-and-minerals/vitamin-b/. Imechukuliwa 14.07.2020 

  2. Vitamin B. better health channel. https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/healthyliving/vitamin-b. Imechukuliwa 14.07.2020

  3. David O. Kennedy. B Vitamins and the Brain: Mechanisms, Dose and Efficacy—A Revie. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4772032/. Imechukuliwa 08.04.2021

  4. R. A. Peters. THE VITAMIN B COMPLEX. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2457859/. Imechukuliwa 08.04.2021

  5. Neuroton. https://www.amoun.com/leap-portfolio-project/neuroton-ampoules-tablet/.Imechukuliwa 08.04.2021

  6. Fiona O’Leary, et al. Vitamin B12 in health and diseses. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3257642/. Imechukuliwa 08.04.2021

  7. Vitamin B9 nutrition facts. https://www.nutri-facts.org/en_US/nutrients/vitamins/b9.html. Imechukuliwa 08.04.2021

  8. Vitamin b9(folic fcid)https://www.hsph.harvard.edu/nutritionsource/folic-acid/. Imechukuliwa 08.04.2021

bottom of page