Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Glory, MD
ULY CLINIC
15 Juni 2025, 08:19:29
Kutokwa na ute mweupe mzito ukeni ni dalili ya mimba?
Ni kawaida kwa mwanamke kutokwa na ute mweupe ukeni usio na harufu kali kabla au wakati wa ujauzito. Hali hii husababishwa na ongezeko la homoni ya estrojeni ambayo huchochea seli za uke kuzalisha ute kwa wingi. Ute huu una faida mbalimbali, ikiwemo kuandaa mazingira salama kwa mbegu za kiume na kusaidia kupambana na vijidudu.
Uhusiano wa ute mweupe na mimba au uovuleshaji
Kutokwa na ute ukeni si dalili ya mimba pekee. Mwanamke anaweza pia kuona ute huu wakati wa kipindi cha uovuleshaji — yaani wakati yai linapokuwa tayari kutoka na kurutubishwa. Kipindi hiki huwa hatari kwa mwanamke kushika mimba endapo atashiriki ngono bila kinga, na hudumu kwa takribani masaa 24 hadi 36.
Sifa za ute mweupe wa kawaida wakati wa ujauzito
Ute huu una sifa zifuatazo:
Rangi nweupe kama karatasi au maji
Hauna harufu au huwa na harufu isiyokera
Awali mzito, baadaye unakuwa mwembamba zaidi
Huzidi kadri ujauzito unavyokua
Sifa za ute mweupe wakati wa uovuleshaji
Ute wa ovulesheni hutofautiana kidogo, ukiwa:
Mweupe kama ute wa yai bichi
Mwembamba, mlaini, na wenye kuteleza
Hauna harufu wala hauna usumbufu
Huwezesha mbegu za kiume kusafiri kwa urahisi kwenda kwenye mfuko wa uzazi
Dalili nyingine za mimba mbali na ute
Kando na ute, ujauzito wa wiki za awali unaweza kuambatana na dalili zifuatazo:
Kukosa hedhi (amenorrhea)
Kichefuchefu au kutapika
Matone ya damu au kutokwa damu kidogo
Kuvimba na kuuma kwa chuchu
Maumivu ya tumbo la chini
Uchovu wa mara kwa mara
Jinsi ya kuthibitisha uwepo wa mimba
Ikiwa unahisi unaweza kuwa mjamzito:
Fanya kipimo cha damu (β-hCG) – Kipimo cha mapema zaidi na chenye uhakika
Fanya Ultrasound ya uke – Huonyesha uwepo wa kijiyai cha ujauzito (gestational sac)
Subiri wiki 2 baada ya ngono kisha fanya kipimo cha mkojo (urine pregnancy test)
Kumbuka: Kipimo cha mkojo hakionyeshi mara moja kama ulibeba mimba kwa siku chache tu.
Kumbuka
Usitumie ute wa uke kama njia pekee ya kugundua mimba. Ikiwa una dalili usizozielewa, wasiliana na mtaalamu wa afya kwa uchunguzi sahihi.
Rejeaza mada:
Planned Parenthood. How much vaginal discharge is normal? Available from: https://www.plannedparenthood.org/blog/how-much-vaginal-discharge-is-normal. Accessed 17 Nov 2024.
ULY Clinic. Dalili za ujauzito. Available from: https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ujauzito. Accessed 17 Nov 2024.
ULY Clinic. Dalili za ujauzito wa wiki moja. Available from: https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/dalili-za-ujauzito-wa-wiki-moja. Accessed 17 Nov 2024.
NHS. Signs and symptoms of pregnancy. Available from: https://www.nhs.uk/pregnancy/trying-for-a-baby/signs-and-symptoms-of-pregnancy/. Accessed 17 Nov 2024.
NHS. Vaginal discharge. Available from: https://www.nhs.uk/conditions/vaginal-discharge/. Accessed 17 Nov 2024.
Pregnancy, Birth and Baby. Vaginal discharge during pregnancy. Available from: https://www.pregnancybirthbaby.org.au/vaginal-discharge-during-pregnancy. Accessed 17 Nov 2024.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
