top of page
Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

ULY CLINIC

15 Juni 2025, 09:16:22

Damu au kinyama mimba ya mwezi mmoja ikiharibika (1).jpg

Unaweza kupata UKIMWI kwa kuchangia chanuo la msusi mwathirika?

Baadhi ya watu wamekuwa wakiuliza swali hili na mengine yanayohusiana na hilo kama yafuatayo:


  • Je kwa njia ya kusuka kwa kutumia chanuo Moja labda na mwathirika wa ukimwi unaweza pata maambukizi?

  • Na kama uyo mtu ndo anaetoa huduma ya kusuka ndo mwathirika wateja mnaweza pata maambukizi?


Makala hii imelenga kujibu maswali hayo


Je, mtu anaweza kupata maambukizi ya VVU endapo atachangia chanuo na muathirika wa UKIMWI?


Kuna majibu mawili ya swali hili, yaani NDIO, na HAPANA


Ili mtu aweze kupata maambukizi ya UKIMWI, kunatakiwa kuwa na mgusano wa majimaji au damu kati ya mwathirika kwenda kwa asiye mwathirika.


Endapo anayetumia chanuo anatumia chanuo la mwathirika, ili aweze kupata maambukizi mambo yafuatayo ni lazima yawepo:


  • Chanuo linapaswa kuwa na damu mbichi au majimaji ya damu kutoka kwenye mwili wa mwathirika(kama kidonda, jeraha au majimaji ya maeneo ya siri) ambayo hayajadumu kwa masaa mengi.

  • Mwili wa anayeambukizwa unapaswa kuwa na jeraha ambalo litakunata na majimaji hayo kutoka kwa mwathirika kupitia Chanuo.


Kama hili limetokea, unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kujizuia na maambukizi

  1. Kunawa kwa maji mengi kwenye eneo lililokutanishwa majimaji yaliyoelezewa hao juu.

  2. Kufika kituo cha kutolea huduma za afya ili kupewa PEP baada ya kufanyiwa vipimo na ushauri.


Mambo ya kufanya ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya UKIMWI kwa wamiliki wa saluni

Mambo yanayotakiwa kufanyika saluni ili kupunguza maambukizi ya UKIMWI.

Tafiti zimeonyesha kuwa maambukiiz ya virusi vya UKIMWI saluni yanaweza kupunguzwa kwa kutumia njia mbalimbali za kutakasa vifaa kama vile

  • Matumizi ya kileo kama spiriti jamii ya ethanol, isopropyl

  • matumizi ya Klorini kama Sodium hypochlorate)

  • Matumizi ka kampaundi ya fenoliki

  • Matumizi ya kampaundi za amonia

  • Matumizi ya iodine

  • Matumizi ya iodophores


Chanuo linaweza kufutwa vema kwa pamba ama kitambaa kilicholowanisha kwenye kampaundi hizo ( zile zinazoruhusiwa kutumika kwa namna hii) au kulowekwa kwa muda wa angalau dakika 10 kabla ya kutumika kwa mtu mwingine.


Njia zingine zinazo ambukiza Virusi vya UKIMWI

Njia zingine za maambukizi ya UKIMWI zimeelezewa kwenye makala nyingine katika tovuti hii ambazo unaweza kuzipata kwa kubofya linki zinazofuata;


Kusoma makala zingine zaidi andika unachotaka kusoma kikifuatiwa na neno ulyclinic kisha tafuta kwenye kurasa ya google utakipata mfano. 'Kuchangia wembe wa mwathirika kunasababisha ukimwi uly clinic' na '

vipele vya ukimwi ulyclinic'


Pia unaweza kubofya na kutazama video za njia zianzoeneza UKIMWI na ie zisizoeneza UKIMWI zifuatazo:


Njia zinazoeneza UKIMWI




Njia zisizoeneza UKIMWI



Rejea za mada hii:
  1. ULY CLINIC. Virusi vya UKIWI vinaishi muda gani? https://www.ulyclinic.com/foramu/majadiliano-na-wataalamu/virusi-vya-ukimwi-huishi-muda-ganiImechukuliwa 30.06.2023

  2. CDC. HIV transmission. https://www.cdc.gov/hiv/basics/transmission.html. Imechukuliwa 30.06.2023

  3. Arulogun OS, Adesoro MO. Potential risk of HIV transmission in barbering practice among professional barbers in Ibadan, Nigeria. Afr Health Sci. 2009 Mar;9(1):19-25. PMID: 20842238; PMCID: PMC2932524.

  4. AOD & HHPU, author. Hairdressing policy. The Department of Alcohol and other drugs And HIV Health Promotion; 2002. Retrieved June 14, 2007, http://www.nsweel.an/docs/des/HAIRDRESSING.doc. [Google Scholar]

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

bottom of page