Makala za forum

Homa kwa mtu mzima: Mwongozo kamili
Mara nyingi hutokana na maambukizi ya virusi au bakteria na inaweza kudhibitiwa nyumbani kwa kutumia paracetamol, kupumzika, na kuongeza unywaji wa maji. Hata hivyo, homa kali au isiyoshuka pamoja na dalili za hatari kama kupumua kwa shida, kuchanganyikiwa, au kutapika kila kitu inahitaji uchunguzi na matibabu ya daktari mara moja.

Kumwaga shahawa zenye damu
Kumwaga shahawa zenye damu kunaweza kuwa dalili ya majeraha au maambukizi katika njia ya uzazi au tezi za uzazi. Ni muhimu kuonana na daktari haraka ili kufanyiwa uchunguzi wa kina na kupata matibabu sahihi, kwani tatizo hili linaweza kuashiria hali inayohitaji tiba ya haraka.

Dawa zinazopelekea ulemavu kwa kichanga
Wakati wa ujauzito, baadhi ya dawa kama Valproic acid, Carbamazepine, Thalidomide, Isotretinoin, na Methotrexate zinaweza kusababisha ulemavu wa viungo, moyo, ubongo, au hata kuharibika kwa mimba. Ni muhimu usitumie dawa yoyote kabla au wakati wa ujauzito bila ushauri wa daktari ili kulinda afya ya mtoto na mama.


