top of page

Boresha Afya yako na Jamii kwa kushiriki Utafiti

Mwandishi:

Mhariri:

Kitengo cha Utafiti na Ubunifu ULYCLINIC

ULY CLINIC

Imeandikwa:

4 Machi 2026, 08:14:16

Boresha Afya yako na Jamii kwa kushiriki Utafiti
Watumiaji wa tovuti ya ULYCLINIC Wanaalikwa Kushiriki Utafiti wa Jukwaa la Afya ya Kidijitali linalotumia AI ya Kiswahili

Tanzania – ULY-CLINIC, kwa ushirikiano na timu ya Korea Kusini, inawaalika watumiaji wake kushiriki katika utafiti unaolenga kuboresha huduma za afya kupitia jukwaa la kidijitali linalotumia Akili Unde (AI) kwa Kiswahili. Ushiriki wako ni wa hiari, lakini ni muhimu kwa kuboresha maisha ya sasa na ya baadaye ya jamii.


Bofya kushiriki tafiti hii muhimu kwako na kwa kwa taifa

Mada ya Utafiti

Uundaji, Utekelezaji, na Tathmini ya Athari ya Jukwaa la Afya ya Kidijitali linalotumia Akili Unde (AI) kwa Kiswahili ili kuongeza uelewa wa Afya miongoni mwa Wagonjwa na Wahudumu wa Afya wa ngazi ya kati nchini Tanzania


Lengo la Utafiti

Utafiti huu unalenga:

  • Kuongeza uelewa wa afya kwa wagonjwa

  • Kuimarisha maendeleo endelevu ya kitaaluma kwa wahudumu wa afya wa ngazi ya kati

  • Kupunguza changamoto za lugha, uelewa mdogo, na upatikanaji wa taarifa sahihi za afya

  • Kuwezesha wagonjwa na watoa huduma kufanya maamuzi sahihi ya kiafya


Kwa kutumia mbinu ya utafiti ya uundaji na uboreshaji, jukwaa litaboreshwa hatua kwa hatua kwa kuzingatia maoni ya watumiaji halisi. Baada ya hapo, litafanyiwa tathmini ya kitaalamu ili kupima urahisi wa matumizi, ukubalifu, na athari zake katika kuongeza uelewa wa afya na maarifa ya kitaaluma.


Matokeo yatatoa ushahidi wa kisayansi kwa watunga sera, wabunifu wa mifumo ya kidijitali, na taasisi za elimu kuhusu namna ya kuendeleza mbunifu wa AI unaofaa kwa nchi zenye kipato cha chini na cha kati.


Programu za elimu na mafunzo ya kiafya katika tafiti

Kwa kuwa utafiti huu unahusisha uundaji, utumiaji na upimaji, mbali na kuandaa makala za kwenye jukwaa(tovuti), tumeandaa programu mbalimbali za mafunzo ili kuwasaidia wagonjwa, watoa huduma za afya na wataalamu wengine ngazi ya kati kujifunza kwa urahisi kuhusu Afya. Kila mada imeundwa kwa lugha rahisi ya Kiswahili na inazingatia uhalisia wa mazingira ya kazi na maisha ya kila siku.


Zaidi ya hayo, tumekuongezea Msaidizi wako Akili–unde (Msaidizi wako AU), ambaye atakupa ufafanuzi wa ziada au majibu ya maswali utakayokuwa nayo kuhusu mada husika. Hii inakupa uwezo wa kujifunza kwa undani na kwa kasi yako mwenyewe.


Mada zote zinapatikana kupitia linki hii: [Bofya hapa kwenda kwenye kurasa]


Baada ya kukamilisha mafunzo husika, mshiriki atatunukiwa cheti maalum cha ushiriki kinachothibitisha kuwa amepata elimu au ujuzi muhimu unaohitajika katika eneo hilo la afya.


Tungependa mshiriki wa tafiti hii aweze kutumia sehemu hii kujifunza kisha kutoa maoni halisi kupitia fomu hii ya utafiti inayopatikana hapa.


Watumiaji wa kawaida washioshiriki programu

Endapo huoni programu ya chaguo lako au unapenda kutumia njia nyingine kujifunza, unaweza kutumia uwanja wa mazungumzo (meseji) uliounganishwa na mfumo huu ili kupata maelezo ya haraka kuhusu masuala ya afya.


Kuingia humo, bofya nukta tatu zilizo upande wa kushoto chini (kama inavyoonekana kwenye pichwa), kisha chagua ULY AI chat; tumia huduma hiyo na baadaye tafadhali toa maoni yako kupitia fomu hii hapa

ree
ree

Ushirikiano na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)

Utafiti huu unachangia:

  • SDG 3 – Afya Bora na Ustawi

  • SDG 4 – Elimu Bora


Kwa nini ushiriki wako ni muhimu?

Tafiti na ubunifu vimebadilisha maisha ya binadamu:

  • Ugunduzi wa simu na baadaye simu janja umebadilisha mawasiliano duniani

  • Teknolojia za Akili Unde (AI) zimeleta mapinduzi katika elimu, biashara, na afya

  • Ugunduzi wa dawa mbalimbali umeokoa mamilioni ya maisha


Hakuna mafanikio haya yaliyotokea bila kushiriki kwa watu katika tafiti. Leo, wewe kama mtumiaji wa ULYCLINIC unaweza kuwa sehemu ya mabadiliko haya.

Kwa kushiriki, unapata:

  • Makala za elimu ya afya

  • Ushauri wa AI kwa Kiswahili

  • Mafunzo mbalimbali ya kitaaluma kwa lugha fasaha ya kiswahili


Ushiriki wako utasaidia kuboresha huduma hizi ili ziwe sahihi, rafiki kwa mtumiaji, na zenye athari kubwa zaidi kwa jamii.


Nani anahitajika kushiriki?

  • Wagonjwa wanaotumia jukwaa kupata elimu au ushauri

  • Wahudumu wa afya wa ngazi ya kati wanaotumia jukwaa kuboresha ujuzi

  • Watumiaji wote wanaotaka kuona huduma za afya za kidijitali zikiboresha


Ushiriki ni wa hiari, na taarifa zote zitahifadhiwa kwa usiri wa hali ya juu na kwa kuzingatia maadili ya utafiti.


Wito kwa Jamii

Hii si tu tafiti ya kitaaluma; ni uwekezaji wa pamoja katika mustakabali wa afya ya Watanzania. Kwa kushiriki, unachangia:

  • Kuboresha elimu ya afya kwa Kiswahili

  • Kuimarisha huduma za kidijitali zinazotumia AI

  • Kuleta ushahidi wa kisayansi unaoweza kuathiri sera za afya nchini


Jiunge nasi na uwe mstari wa mbele katika safari hii ya mabadiliko!


Imetolewa kwa Umma

Kitengo cha Utafiti na Ubunifu – ULYCLINIC Platform

Idhini na Ukaguzi:

  • Watafiti wakuu: 김도환 (Dohwan Kim), Sospeter Benjamin Mangwella

  • Protokali Na: IRB-2025-0369

  • Kibadi Na: KUIRB-2026-0025-01

  • Muda wa tafiti: 2026-01-20 hadi 2027-01-19

  • Bodi ya Idhini: Chuo Kikuu Korea


Bofya kushiriki tafiti hii muhimu kwako na kwa kwa taifa

Imeboreshwa

7 Machi 2026, 04:50:29

bottom of page