Mwandishi:
Mhariri:
Imeandikwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
19 Oktoba 2026, 16:45:08
Mwongozo wa kitiba kwa Wataalamu wa Afya

Jipya Kwa Wataalamu wa Afya: Tumia Clinical Bot Kupitia ULY Clinic AUPata Rejea za Matibabu
Katika kuendelea kuboresha na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za kitabibu, ULY Clinic inawataarifu wataalamu wote wa afya kuwa sasa wanaweza kutumia mfumo wa Clinical Bot kupitia ULY Clinic AI hapa hapa kwenye tovuti yetu.
Mfumo huu umeundwa maalum ili kumpa mtaalamu wa afya marejeo ya haraka na sahihi ya kimatibabu kulingana na Mwongozo wa Taifa wa Matibabu (Tanzania Standard Treatment Guidelines - STG 7th Edition, 2026)Â na vyanzo vingine rasmi vilivyoidhinishwa.
Jinsi ya kutumia Clinical Bot
Bofya Kitufe cha Meseji:Â Bonyeza kitufe cha meseji kilichopo chini kwenye tovuti hii.
Chagua Mtaalamu wa Afya:Â Ndani ya dirisha la meseji, bofya kitufe kilichooandikwa "Mtaalamu wa Afya".
Ingia kwenye Akaunti (Login):Â Mfumo utakutaka kuingia kwa kutumia barua pepe yako ili kuhakiki na kulinda usalama wa matumizi ya kitaalamu.
Endelea na Matumizi:Â Mara baada ya kuingia, unaweza kuanza kuuliza maswali yoyote ya kitabibu kama vile miongozo ya utambuzi, vipimo vya dawa, na usimamizi wa wagonjwa kwa kutumia lugha ya Kiingereza kwa sasa.
Faida kuu za mfumo huu:
Upatikanaji wa Haraka:Â Kupata majibu ya moja kwa moja bila kupoteza muda wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa.
Miongozo ya Hivi Karibuni:Â Inazingatia kikamilifu miongozo mipya ya STG 2026.
Urahisi wa Matumizi:Â Unaweza kuitumia ukiwa kwenye kompyuta au simu yako ya mkononi.
Kanusho la Kitaalamu:Â Mfumo huu umelenga kutoa taarifa kwa ajili ya mafunzo, elimu, na marejeo ya kitaalamu pekee. Wataalamu wa afya wanapaswa kutumia weledi wao binafsi wa kitabibu na kuhakikisha usahihi wa vipimo kabla ya kutoa matibabu kwa mgonjwa.
Imeboreshwa
19 Oktoba 2026, 16:45:08

