Adrenalini (Epinefrini) ni homoni na dawa inayotolewa na tezi za adreno ambayo huandaa mwili kupambana au kukimbia wakati wa hatari kwa kuongeza mapigo ya moyo, sukari ya damu na mtiririko wa damu kwenye misuli.
Insulin ni homoni inayotengenezwa na kongosho inayofanya kazi ya kuruhusu sukari aina ya glukosi iingie kwenye seli na kuipa nguvu ifanye kazi au kuhifadhi sukari hiyo ili itumike baadae. Mbali na kazi hiyo muhimu, insulin pia hufanya kazi ya kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.