Huduma ya kwanza
Katika sehemu hii utajifunza kuhusu huduma ya kwanza kwenye matukio mbalimbali ili uweze kuwa msaada pale itakapohitajika kabla wataalamu wa afya hawajafika kwenye tukio

Kupunguza msongo wa mawazo kwa Upumuaji wa kina: Mwongozo kamili
Mbinu za kupumua kwa kina kama 4-7-8, upumuaji wa tumbo, upumuaji mraba, upumuaji wa kubadili tundu la pua na upumuaji makinifu husaidia kudhibiti hisia, shinikizo la damu, na usingizi. Kutumia moja ya njia hizi kila siku hufanya akili na mwili kuwa tulivu, kuongeza umakini, na kupunguza hisia za wasiwasi, hofu, au mfadhaiko zinazotokea ghafla.

Muda wa kutoa nyuzi za upasuaji
Nyuzi za kidonda, ni nyuzi laini zinazoshonwa kwenye kidonda ili kukutanisha kuta za kidonda ili kiweze kupona. Nyuzi zinaweza kuwa za kuyeyuka au zisizo za kuyeyuka, nyuzi za kuyeyuka mara nyingi huyeyuka ndani ya wiki 4 hadi 8. Nyuzi za kuyeyuka huwa hazihitaji kutolewa kwenye kidonda kwa kuwa huyeyuka zenyewe.

Matibabu ya maumivu ya koo
Maumivu ya koo ni dalili ya hisia za kuhisi maumivu, ukavu au kukwanguliwa kwa koo. Tatizo hili huwapata watu wengi duniani.
Mara nyingi maumivu ya koo husababishwa na maambukizi ya virusi na hewa kavu kwenye mazingira na mara nyingi dalili hii hupotea yenyewe bila matibabu.


