top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeandikwa:

Dkt. Adolf S, MD

Dkt. Benjamin L, MD

23 Septemba 2022 06:08:03

Cotrim

Cotrim ni jina la kibiashara la dawa inayojulikana kama co-trimoxazole ambayo nii mchanganyiko wa dawa aina mbili yaani sulfamethoxazole na trimethroprim.


Cotrim hutumika katika matibabu ya magonjwa mbali mbali yanayosababishwa na bakteria, fangasi na protozoa, na pia tumika kama kinga dhidi ya magonjwa nyemelezi kwa watu waishio ya Virusi vya Ukimwi.


Uzito wa cotrim


Cotrim hupatikana katika mfumo wa vidonge, dawa ya maji na sindano katika uzito ufuatao


Vidonge

 • Cotrim 400 mg/80 mg (humaanisha sulfamethoxazole 400 mg na trimethroprim 80 mg)

 • Cotrim 800 mg/160 mg (humaanisha sulfamethoxazole 800 mg na trimethroprim 160 mg)


Dawa ya maji

Cotrim 200 mg/40 mg) 5 mls (yaani sulfamethoxazole 200 mg na trimethroprim 40 mg katika ujazo wa mlilita 5)


Sindano

Cotrim (80 mg/16 mg) /ml (yaani sulfamethoxazole 80 mg na trimethroprim 16 mg katika ujazo wa mlilita)


Wapi unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu cotrim


Soma zaidi kuhusu septrin; magonjwa inayotibu, maudhi yake na maelezo mengine kwenye mada inayohusu Co-trimoxazole


Majina mengine ya kibiashara ya cotrim


Majina mengine yanayotumika katika makampuni ya kuzalisha dawa yanayomaanisha septrin ni kama ifuatavyo

 • Actrim

 • Bactrim

 • Bactrim DS

 • Septrin

 • Septra

 • Septra DS

 • Cotrim

 • Cotrim DS

 • Sulfatrim

 • Sulfatrim DS

Uly clinic inakushauri siku zote wasiliana na daktari wako kwa ushauri wa matumizi ya dawa yoyote. Usitumie dawa bila kushauriwa na daktari ili kuepuka madhara na kufanya vimelea kuwa sugu kwenye dawa.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia linki ya 'Pata tiba' au 'Wasiliana nasi' chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii:

Imeboreshwa:

23 Septemba 2022 06:08:24

bottom of page